Ugonjwa huu hushambulia karibia mifugo yote na pia binadamu, kwa
binadamu ugonjwa huu hujulikana kama malale. ugonjwa huu husababishwa na
vijidudu vya protozoa vijulikanavyo kama Trypanosoma evansi na kusambazwa na mbung'o au ndorobo (glossina spp)
vijidudu hivi vikimuingia mnyama vinatumia kiasi kingi cha sukari
kwenye mwili wa mnyama na kuharibu seli nyekundu za damu na
kusababisha upungufu mkubwa wa damu kwa mnyama.
DALILI
1- Ugonjwa huu kwa ng'ombe unaweza kuwa wa hatari na hata kuwa sugu na kuleta madhara makubwa ikiwamo kifo
2 -Joto la mnyama hupanda hadi kufikia sentigredi 39 - 41
3 -Mnyama hupata tabu kuona huku akitoa machozi mengi kama anayelia
4 -Uzalishaji wa maziwa hupungua ghafla kwa kiasi kikubwa
5 -Mnyama hupumua kwa tabu kwa kutumia nguvu
6 -Mnyama huonyesha kuchanganyikiwa akili, anaweza kutembea kwa mduara, kupiga piga kichwa kwenye mabanda au chochote na mnyama huweza kupoteza fahamu
7 -Baadhi ya wanyama wajawazito huweza kutoa mimba, hii ni kwenye ile hali ya ugonjwa sugu ambao hushambulia pole pole
8 -Kuvimba kwa matezi
9 -Manyoya ya ng'ombe mgongoni wakati wa asubuhi yana kuwa yanang'aa kwa aina fulani jua likiwaka, ila inahitaji uonyeshwe na wataalam kwanza
NG'OMBE AINA YA N'DAMA

UCHUNGUZI
Maafisa ugani wa mifugo watachukua sampuli za damu kutoka kwenye mkia au sikio la mnyama na vijidudu kuonekana kwa darubini ya umeme mkali kabla ya damu kukauka, pia njia ya kimaabara ya GIEMSA itasaidia
kwa uchunguzi zaidi wa kimaabara wadudu wanaweza kupandikizwa kwenye sungura, panya na simbilisi/pimbi na baadae njia ya PCR, ELISA kutumika kuangalia vichochezi vya mwili
TIBA
Kwa mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, jamii ya farasi, mbwa na paka dawa kama diminaphen, diminakel hutumika kutibu ugonjwa huu, kwa upande wa binadamu sifahamu dawa gani inatumika
KINGA
1 - Kuna njia ya kitaalam ijulikanayo kama sterile male technique, ambapo madume ya mbung'o hupigwa na mionzi ya gama na kushindwa kuzalisha yanapo panda, hii husaidia sana kwa sababu majike ya mbung'o hupandwa mara moja tu katika maisha yao wakati madume haya tasa huendelea kupanda majike tofauti tofauti
2- Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu zinaweza kukinga wanyama kama watapigwa kila baada ya miezi mitatu na mara 4 kwa mwaka
3- Kuna jamii ya ng'ombe wanaojulikana kama N'DAMA ambao hupatikana Afrika ya magharibi, aina hii ya ng'ombe inastahimili sana ugonjwa huu
No comments:
Post a Comment