Wednesday, January 21, 2015

JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI

Tengeneza chakula cha samaki mwenyewe

PAGE 7Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.


Mahitaji


• Pumba ya mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.

Namna ya kuandaa


• Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.

14 comments:

  1. naomba kuuliza nataka chakula cha samaki kisicho zama chini

    ReplyDelete
  2. ukiwa m
    na samaki 1300 wa kambale wanapaswa kulishwa kiasi gani
    ya chakula hicho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Samaki hulishwa kulingana na uzito wao, kama ni wadogo hulishwa 5% ya uzito wao na kadri wanavyoongezeka uzito kiwango hupungua mpaka 3%. Mfano hao kama ni wakubwa kuanzia uzito wa 500gm unatakiwa kuwalisha 19.5kg kwa siku ambayo hiyo ni 3% ya jumla ya uzito wao..nimechukulia wastani wa uzito wa kila mmoja ni 500gm.ASANTE.

      Delete
    2. Samaki hulishwa kulingana na uzito wao, kama ni wadogo hulishwa 5% ya uzito wao na kadri wanavyoongezeka uzito kiwango hupungua mpaka 3%. Mfano hao kama ni wakubwa kuanzia uzito wa 500gm unatakiwa kuwalisha 19.5kg kwa siku ambayo hiyo ni 3% ya jumla ya uzito wao..nimechukulia wastani wa uzito wa kila mmoja ni 500gm.ASANTE.

      Delete
    3. Mimi nataka kifahamishwa jinsi yakutengeneza samaki wa mapambo

      Delete
  3. Mnatisha na je kama hunakisagio unatengeneza je

    ReplyDelete
  4. Enter your comment...mm kwa habari ya tambi sina shida ila zinazama nataka kujua nizifanyeje zielee?

    ReplyDelete
  5. Kwa chakula cha Samaki kizuri na ambacho hakizami kwenye maji na hata hakichafui maji huduma tumia chakula cha Azolla na kwa huduma za Chakula cha Azolla tunatoa huduma hizo kupitia kampuni yetu ya AZOLLA FEEDERS SUPPLY Co. LTD kwa mawasiliano yetu ni 0712350111/0757737124

    ReplyDelete
  6. Bei ya chakula cha samaki kwa kilo ni shiling ngap hasa kwa dar?

    ReplyDelete