Friday, July 28, 2017

Ndugu wanablog wa wakulima na wafugaji

Habari ya siku nyingi!! Kwa kweli tumepotea kwa muda mtatuwia radhi wadau wetu wa kilimo na wafugaji.

Tuna mambo mazuri sana ndugu zetu tunataka kuwaletea ambayo ni kilimo na ufugaji,Tukianza na kilimo, mwaka huu baadhi ya maeneo ya nchi yetu.yamepata mvua nzuri na mengine ya wastani na mengine hayakupata kabisa. Hivyo basi tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwani mwaka jana msimu kama huu hali ikikuwa tete kidogo ya chakula, sasa basi ninaipongeza serikali kwa uhamuzi wake kwa kuliona hilo tatizo iliyotupata mwaka jana ya kuchukua hatua ya kuzibiti chakula kisitoke nje ya nchi bila kibali.

Napenda kuchukua fursa hii kwa kuwakumbusha wadau wote wa kilimo kutunza hii kitu kilicho kipata mwaka kwa uangalifu mkubwa, Hivyo basi shime wadau wa kilimo tushirikiliane na serikali katika tafiti mbalimbali za kilimo cha kisasa pamoja na umwangiliaji,  hitatusaidia kuwa na mazao mengi kwa technology ya kisasa kwa mfano sasa zipo taasisi nyingi zinazoamasisha matumizi ya green house

Napenda wadau wote wa kilimo tushirikiane kwa pamoja ili tuwe na chakula cha ziada hata kuweza kuuza nje ya nchi yetu na kuachana na dhana ya kutengemea mvua za masika nk.

Kwa upande wa mifugo nayo lazima tutumie technology ya kisasa ya ufugaji wa zero graize ambao huu utamzuia mfugaji kuzungunga na mifungo toka kaskazini hadi kusini na kufanya kutulia sehemu moja.

Na hii itafanya kuwa na mifugo yenye tija na ufugaji wenye tija  sana kwa maendeleo ya mfugaji na taifa pia.Sisi kama taasisi isiyo kuwa ya kiserikali tupo tayari kutoa elimu na kuonganisha wadau wote wa pande zote mbili wa wakulima na wafugaji tukishirikiana na serikali.

No comments:

Post a Comment