Muhtasari
wa ufugaji kuku wa asili ili kuzuia vifo na kuboresha uzalishaji.
Ufugaji
wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa
kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji
kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili watanzania
wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama
sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa
huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa
mbali mbali . muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili
uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku
kwa wingi.
Dondoo ya 1. Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
·
Uchafu ni
mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya
·
Vyombo
vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji na sabuni.
Pumba au
chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku vitolowe na kuzikwa.
·
Choma
moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
·
Usifuge
kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
·
Ondoa
mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
·
Tumia
dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa
mwaka.
·
Ziba
matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia
katika banda la kuku.
Dondoo ya 2. Magonjwa na kinga kwa kuku wote.
Ndui ya kuku.
Huathiri
sana vifaranga wanaokua na kujitokeza kwa wingi wakati wa mvua ndefu.
Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na
manyoa.
Mdondo/kideri
Mdondo,
au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari kuliko kati ya
magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika
zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
Ukosefu wa vitamin A
Ugonjwa huu
husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni iliyolowana. Kuku
wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi
kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.
Koksidiosisi
Huathiri
kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokuwa. Kuku
hudhoofika manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha
damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.
Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni
wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na
kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu.
Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga
na kuatamia.
Minyoo.
Minyoo
huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi.
Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.
Dondoo ya 3. Chakula cha ziada:
·
Wapatie
vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya
dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.
·
Changanya
kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia
kikombe kidogo cha chai) .
·
Mchwa na
wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.
·
Vuna
mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.
·
Kutengeneza
mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au
maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.
·
Mwagia
maji hadi kila kilichomo kirowane kasha weka katika chombo kama ndoo au
chunngu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri
hadi kesho yake asubuh, kasha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali
walipo.
Dondoo ya 4. Utotoleshaji wa vifaranga;
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku .
·
Sifa za
jogoo bora ;
1. Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia
upande mmoja.
2. Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye
sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo
wawili wanatosha.
·
Sifa za
tetea bora;
Tetea
bora ni Yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha,
kuatamia na hatimae kutotoa vifaranga na
·
Uhiffadhi
wa mayai;
1. Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
2. Tuma box lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na
safi au kasha la kuhifadhia mayai.
3. Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile
iliyochongoka itizame chini.
4. Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
5. Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja
liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
·
Kuatamiza
mayai;
-
Kuku
awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.
-
Mayi 10
hadi 12 yanatosha kutamia.
-
Mayai ya
kutamiza yasizid wilki 2 toka kutaga.
-
Yai la
mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na
apewe kuku kuyaatamia.
-
Mayi ya
kutamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu
na safi au kilichowekwa spiriti
·
Kutotolesha
vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
-
Kama
unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;
-
Kuku wa
kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa
kisasa au kuku asiye na jogoo.
-
Rudia
zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kasha waweke kuku wote mayai yenye
mbegu.
Dondoo ya 5. Matumizi ya vifaranga ili kuzuia vifo.
Vifaranga
wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na
kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifarang wa siku 1 hadi miezi
miwili zingatia yafuatayo;
Ulinzi
dhidi ya mwewe na wanyama wengine.
Weka vifaranga
kwenye tenga na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na
chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale
na mama yao.
Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama
tetea alichanjwa kabla ya kuanzakutaga vifaranga wanaoambuliwa huwa na kinga ya
mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao
dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga
ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu
baada ya kuanguliwa, rudia wakifikisha wiki tatu kasha uchanje kila baada ya
miezi 3
Kinga
dhidi ya kiksidiosisi
Kinga ya
koksidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.
·
Wape dawa
ya aprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea
waanguliwe kama kinga ya koksidiosisi.
·
Dawa
inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya
kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa
katika maji au pumba
·
Kama
vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvua koti wapewe dawa ya
amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;
Dawa siku
tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu
HITIMISHO
Hakikisha
banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.
·
Usichanganye
kuku na bata katika banda moja
·
Lisha
chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
·
Kideri,
koksidiosisi, ndui na upungufu wa vitamin
A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako
dhidi ya magojwa haya.
·
Kumbuka
kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
·
Vifaranga
wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri fuata maelezo kuzuia vifo.
·
Kumbuka
ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga
kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.
·
Muone
mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.
·
Soma
maelezo haya mara kwa mara na ufanye yalioelekezwa.
·
Washirikishe
wengine katika kaya yako ili nao wajifunze na kufanya, ivyo kukuza ufugaji na
kipato cha familia.
No comments:
Post a Comment