Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili
ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa
ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki
kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya
hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya
2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya
mkataba na kampuni hiyo.
Hoho hutumika katika kutengeneza rangi
za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile
zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula.
Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya
nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso
n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya
chuma, vitamin A na C.
2.0 TABIA YA MMEA
Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,.
3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO
Hoho
hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita
2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi
za sentigredi 21 hadi 24. Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha
maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi.
Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache.
4.0 UZALISHAJI
4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU
Chagua
eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha.
Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili,
biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na
magonjwa.
Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri
matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa
mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja. Acha
njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku
moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya
hewa na hali ya udongo. Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari
na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo
kinatosha eneo la hekta moja. Weka matandazo kwenye kitalu au tumia
nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu.
4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba
lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na
kurahisisha umwagiliaji. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo
kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili
na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.
4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU
Mbegu
ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za
kilimo nchi nzima. Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu
uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko
unashauriwa kununua mbegu bora.
4.4 UPANDAJI
Mbegu
huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche
hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni
kabla ya kuhamisha miche. Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya
miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana
kwa hekta. Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya
kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa
hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha.
5.0 KUHUDUMIA SHAMBA
Palizi
ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike
kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo
140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata
matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).
6.0 MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu
• Funza wa vitumba
• Vidukari
• Kidomozi (Leaf miner)
Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin
Magonjwa
• Kuoza mizizi
• Mnyauko wa majani
• Batobato
Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu.
Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili.
7.0 UVUNAJI
Matunda
ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa;
matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa.
Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.
Ubora wa hoho huongezeka
kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani.
Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia
maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji
unaofuata.
8.0 USINDIKAJI
Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.
9.0 SOKO LA PAPRIKA
Soko la
hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho
hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia
kwenye kachumbari. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni
kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza
shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua
zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi
Kuna aina ya pilipili
isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida
ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi. Zao hili kwa
sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa
Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa
No comments:
Post a Comment