Wakulima wa zao la korosho mkoani Lindi wamepata hasara ya jumla
ya Sh10 bilion kutokana na kuuza korosho kwa bei ya chini ya dira ya
Sh1200.
Kufuatia hasara hiyo wakulima hao wameitaka
Serikali iwafidie wakulima hao wa korosho kama ilivyo kwa wakulima
wengine ambao huwa wanapata hasara nchini.
Hayo yalibainishwa mkoani hapa na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Abdallah Chikawe ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Lindi (ALAT),
wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Chikawe alisema wakulima wa zao la korosho wa Mkoa
wa Lindi hawana imani na Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Lindi cha
Ilulu pamoja na COASCO.
Hata hivyo walimtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi afunge
akaunti zote za Chama cha Ushirika cha Ilulu cha mkoani Lindi hadi hapo
ukaguzi utakapofanywa .
No comments:
Post a Comment