Hotuba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher
Chiza imezidi kupingwa kwa madai kuwa imejaa majibu ya uongo kwa
Watanzania.
Licha ya suala hilo, kitendo cha Waziri Chiza
kupeleka mradi wa bwawa la umwagiliaji Wilaya ya Kakonko ambako ndiko
jimboni kwake, kilionekana kuwakera wabunge.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika juzi, Mbunge wa Viti Maalumu, Azzah Hilali (CCM) alisema
Hotuba ya Waziri Chiza ilitolewa bungeni bila ya kufanyiwa utafiti wa
kutosha, kwani vitu vingi vinaonekana havina uhalisia.
“Mambo mengi hapa ya Waziri hayana ukweli, kwani
unaposema chakula hutolewa kwa wananchi mara baada ya wakurugenzi kuleta
maombi siyo kweli,” alisema Hilali.
Alisema tangu Oktoba mwaka jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, aliomba chakula cha msaada lakini kilipelekwa nusu Februari mwaka huu.
Alisema tangu Oktoba mwaka jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, aliomba chakula cha msaada lakini kilipelekwa nusu Februari mwaka huu.
Pia, Mbunge huyo alikosoa hotuba hiyo kuwa
imetumia jina la Waziri Mkuu vibaya, kwani kiongozi huyo aliagiza
chakula cha msaada kupelekwa Shinyanga tangu muda mrefu, lakini hakuna
kitu chochote kilichofanyika.
“Ndiyo maana tunasema mnadanganya, wewe fikiria
hata hao wataalamu wenu mnaowatuma wanaishia maofisini, huku mnakuja
kutoa taarifa kuwa wamefika huko na kufanya kazi, jamani Watanzania
wamechoshwa kudanganywa,” alilalamika.
Kuhusu mradi wa bwawa la Kakonko, Mbunge huyo
alimtuhumu moja kwa moja Waziri Chiza kuwa anapanga miradi ya maendeleo
kwa upendeleo.
Alisema Serikali ilitangaza Kahama kuwa italisha
Mkoa wa Shinyanga, lakini hakuna mradi hata mmoja ulioelekezwa wilayani
humo, badala yake miradi imepelekwa maeneo yenye neema ya mvua na kuhoji
dhambi waliyomfanyia Mungu.
No comments:
Post a Comment