"Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika akitoa hotuba kwa Wadau wa Sukari katika Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro Mwanzoni mwa Januari 2014.
Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza (Mb)
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika ameonya kuwa kuwa Serikali
haitapenda kuona Tasinia ya Sukari ikikosa mweleleo kutokana na matakwa
ya kundi fulani. Alisisitiza kuwa, Tasnia ya sukari ni moja ya tasnia
kubwa nchini ikijumuisha wadau muhimu wakiwamo walaji, wakulima,
wafanyabiashara na wazalishaji. Kila mdau katika jumuisho hili ana
maslahi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kukinzana na ya
mdau mwenzake. Mkulima angependa kuona anauza miwa yake kwa bei ya juu,
hali kadhalika mzalishaji kuuza sukari anayozalisha kwa bei yenye
faida ya kutosha. Aidha mfanyabiashara angependa kupata faida maradufu
na panapokuwa na mwanya kuingiza sukari kutoka nje kwa njia sizizo
halali. Lakini kwa upande mwingine mlaji naye angependa kununua sukari
kwa bei nafuu.
Serikali haipo
tayari kuona tasnia kubwa na muhimu kama hii ya sukari ikipoteza
mwelekeo, aidha ingependa kuwepo kwa mazingira mazuri (win - win situation)
kwa kila mdau. Kwa maana hiyo nimeona ni jambo jema na muhimu sana
kuwakutanisha ninyi wadau ili tuweze kujadili kwa pamoja changamoto
zilizopo mbele yetu juu ya sekta hii. Ni matarajio yangu kwamba,
mkutano huu utaweka misingi ya kufikia utatuzi wa chamngamoto hizi kwa
manufaa ya pande zote
Mhe. Waziri ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa Sukari uliofanyika Mjini Morogoro mwanzoni wa mwezi Januari
Akitoa picha
halisi ya uzalishaji na mahitaji ya sukari hapa nchini Waziri Chiza
alisema kuwa, Wakati viwanda vyetu vinabinafsishwa vilikuwa vinazalisha
wastani wa tani 120,000 kwa mwaka. Sasa uzalishaji umefikia wastani wa
tani 300,000 kwa mwaka.
Aidha uzalishaji
wa miwa (siyo sukari) katika mashamba ya wakulima wadogo nao
umeongezeka kwa asilimia 61 (hii ni kutoka wastani wa uzalishaji wa
tani 439,122 hadi tani 705,176 kwa mwaka). Uzalishaji katika mashamba
ya wenye viwanda umeongezeka kutoka wastani wa tani 1,083,738 na
kufikia tani 2,229,274 kwa mwaka (ongezeko la asilimia 105).
Pamoja na
mafanikio haya bado tasnia ya sukari imegubikwa na changamoto mbali
mbali kubwa zaidi ikiwa uzalishaji usiokidhi mahitaji. Mahitaji yetu
ni wastani wa tani 590,000 za sukari kwa matumizi ya kawaida na ya
viwandani. Viwanda vya sukari nchini huzalisha takribani asilimia
sabini tano (75%) ya mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida. Wastani
wa tani 290,000 ni nakisi inayojazwa na uagizaji sukari kutoka nje.
Nakisi hii inajumuisha sukari ya matumizi ya kawaida (gap sugar)
ya wastani wa tani 120,000 na sukari ya matumizi ya viwandani ya
wastani wa tani 170,000 kwa mwaka. Kiasi chote cha sukari ya matumizi
ya viwandani kinaingizwa nchini kutoka nje. Aidha uagizaji wa sukari ya
matumizi ya kawaida unategemea hali halisi ya soko kwa kipindi husika
na kwa hiyo uagizaji halisi unaweza kuwa juu au chini ya nakisi hiyo.
Hata hivyo, Kamati ya Ufundi ya Ushauri ya Uagizaji Sukari iliyokutana
tarehe 24/12/2013 kujadili hali ya sukari nchini imependekeza kuwa
mwaka huu 2013/2014 kusiwe na uagizaji wa sukari kwa sababu kiasi tha
tani 257,000 kitapatikana kwa matumizi ya kawaida kuanzia sasa hadi
mwishoni mwa 2013/2014.
No comments:
Post a Comment