Tuesday, January 27, 2015

Kuanzisha mradi wa mbuzi wa maziwa

Kuanzisha mradi wa mbuzi wa maziwa

Watu wengi hutemea mifugo kwa riziki.Ufugaji wa wanyama humpa mkulima nyama na maziwa kwa matumizi ya nyumbani na mapato kutokana na mauzo ya ziada. Mifugo pia ni chanzo cha samadi. Bidhaa zingine za wanyama zinazoweza kuuzwa ili kupata pesa zinajumulisha ngozi,samadi ya kuongeza rutuba kwenye ardhi ya kupanda mimea na pia kutoa kawi ya biogas, pembe, kwato na midomo ya ndege. Kuna aina mingi ya wanyama ambao mkulima anaweza kuwafuga kuanzia kwa ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia na vile vile ndege wa nyumbani kama kuku, bata bukini, bata na mbuni.


 Chaguo la mnyama wa kufuga hutegemea mambo mengi. Hata hivyo wakulima wengi hufuga wanyama ambao wana ujuzi wa kuwasimamia na wanawapatia mapato mazuri. Mbuzi wa maziwa hummtolea mkulima maziwa ya kunywa na kuuza,na samadi ya kurutubuisha ardhi na mbuzi wenyewe wanaweza kuuzwa. Na kipato cha ziada,wakulima wanaweza kulipa ada za nyumbani; kuwapeleka bwatoto wao shuleni ama kuwekeza mara nyingine kwa shamba na biashara zingine. Uchunguzi kifani unaofuata unaonyesha jinsi ya kufuga mbuzi wa maziwa,yaani kwa minajili ya utoaji wa maziwa.Msingi wake ni mradi unaoendelea katika divisheni ya Kibwezi katika wilaya ya Makueni ambao unafanywa na wenyeji na usaidizi wa shirika lisiilo la kiserikali linaloitwa Farm-Africa.  Shirika hili lisiilo la kiserikali lilianzisha mradi uliotoa kizazi cha mbuzi kilichoboreshwa kinachoitwa Toggenburgs. Mbuzi hawa ambao ni wa kiume ni wa uzalishaji mtambuka na vizazi vya mbuzi wa kienyeji. Mradi huu pia umewapa mafunzo wakulima na wafanya kazi wa nje kuhusu ujuzi wa kufuiga mbuzi na kuwasimamia.Mafunzo haya yanajumlisha sehemu zifuatazo.
  • Jinsi ya kufanya uzazi na kuchagua mbuzi ili kuzalisha maziwa mengi na bora .
  • Mbinu bora za ulishaji na shughuli za lishe.
  • Jinsi ya kujengea wanyama makaazi bora ya kuwalinda dhidi ya hali ya hewa na tabia ya nchi.  
  • Jinsi ya kuboresha usafi wa maziwa na bidhaa za maziwa.
  • Jinsi ya kudhibiti vimelea wa nje na ndani ambayo husababisha afya mbaya na hupunguza utoaji wa maziwa.
  • Jinsi ya kuuza bidhaa za mbuzi wa maziwa kama maziwa.
Njia moja ambayo watu katika jamii wanaweza kanzisha ufugaji wa mbuzi wa maziwa ni kwa kujikusanya katika vyama vya jamii ambavyo vina haja ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa.Kikundi kinaweza kumpata mbuzi aliyeboreshwa ambaye huwa ni wa kiueme ili ajamiane na mbuzi wa kike wa kienyeji ambaye huzaa mbuzi wenye afya anayekuwa haraka. Njia nyingine ni kununua mbuzi wa uzalishaji mtambuka kutoka kwa wakulima wengine ambao tayari wana mbuzi hawa. Ili kuwasimamaia barabara mbuzi wao wa maziwa,wanajamii watahitajika kupewa mafunzo katika sehemu zilizoelezwa hapo juu. Haya yanaweza kufanywa kwa kujifunza kutoka kwa wakulima ambao tayari wanajishughulisha na ufugaji wa mbuzi wa maziwa kwa mfano wale wa Kibwezi.

posted by Elias w eastern Grade farm

No comments:

Post a Comment