Dar es Salaam. Imeelezwa kwamba wakulima wa Korosho nchini wataendelea kupata mapato duni hadi hapo Serikali itakaposaidia uwekezaji wa viwanda vya ubanguaji wa korosho katika mikoa inayolima zao hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya
Kuondoa Umaskini (Repoa), Profesa Samwel Wangwe alisema juzi kwamba
uuzaji wa korosho zisizobanguliwa nje ya nchi ni hasara kwa wakulima.
Profesa Wangwe alisema hayo wakati wa majadiliano
ya utafiti unaolinganisha ufanisi wa zao hilo kati ya Tanzania na
Vietnam uliofanywa na Dk Blandina Kilama wa Repoa.
“Tunahitaji kuongeza thamani ya zao hili kwa
kujenga viwanda vya kisasa vya kubangua korosho ili tuweze kuuza kwa
thamani itatayowanufaisha wakulima,” alisema Profesa Wangwe.
Wakati Profesa Wangwe akisema hayo, viwanda vya
kubangua korosho ambavyo Serikali ilibinafsisha kwa watu binafsi,
vimegeuzwa maghala ya kuhifadhia mazao na kusababisha korosho kuuzwa
zikiwa hazijabanguliwa.
Kwa upande wake, Dk Kilama alisema katika utafiti
wake kwamba ingawa Tanzania ilianza kilimo cha korosho kabla ya Vietnam
lakini nchi hiyo iko juu kiuzalishaji kuishinda Tanzania.
Alisema kinachowasaidia ni kwamba mbali na
Serikali hiyo kuweka sera bora za kilimo, pia kuna viwanda vingi vya
kubangua korosho hali inayowafanya waongeze thamani ya zao hilo.
“Hata Bodi ya Korosho ya Vietnam inajumuisha
wataalamu wa kilimo, wakulima na wabanguaji jambo ambalo ni tofauti hapa
kwetu ambapo bodi inaweza kuwa na watu ambao siyo wadau wa korosho,”
alisema na kuongeza kwamba Tanzania imeshuka kwa kiasi cha kutisha
katika uzalishaji zao
No comments:
Post a Comment