Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Pamba Tanzania
(Tacoga), Elias Zizi amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuhujumu kilimo
cha zao.
Zizi anashtakiwa kwa kununua pamba kabla ya msimu, ikiwamo kufanya biashara ya pamba bila leseni.
Mwendesha Mashtaka Polisi, Clement Kitundu
alidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alikamatwa May 6, mwaka huu
Kijiji cha Mbiti, Kata ya Mango, wilayani Bariadi, akinunua pamba.
Kitundu alidai kuwa suala hilo ni kosa tena bila
leseni. Ilidaiwa kuwa kwa vipindi na siku tofauti, mshtakiwa ambaye ni
kiongozi wa chama cha wakulima anayetambua na kuelewa sheria na kanuni,
alitenda kosa hilo na kufanikiwa kununua zaidi ya tani moja ya pamba kwa
nia ya kuiuza baadaye.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa
dhamana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Bariadi, Robert Oguda
aliamua mahakama kuhamia eneo la tukio kupima na kushuhudia pamba hiyo
ikiwamo kupima uzito, kazi iliyofanyika chini ya usimamizi wa polisi.
No comments:
Post a Comment