Friday, February 27, 2015

Matrekta 3000 kuingizwa nchini

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO
KAMPUNI ya kutengeneza Matrekta iitwayo ARSUS ya nchini POLAND, inatarajia kuingiza Matrekta elfu tatu (3,000) kwa kushirikiana na kampuni ya SUMA JKT ili kukuza sekta ya kilimo hapa nchini

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO ameiambia TBC mjini BERLIN UJERUMANI, kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya kilimo, ni matokeo ya kuvutia uwekezaji wa eknolojia na mitaji kutoka nje unaofanywa kupitia uwakilishi wa diplomasia ya kiuchumi

Sekta ya kilimo nchini Tanzania inaajiri zaidi ya asilimia 85 ya watanzania hususani waishio vijijini.

Changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni pamoja na matumizi duni ya zana za kilimo hali iliyoifanya Tanzania kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuimarisha sekta hiyo.

Akizungumzia sekta ya utalii, BALOZI PHILIP MARMO amesema kuwa idadi ya watalii kutoka nchi za Ulaya wanaotembelea Tanzania imeongezeka hadi kufikia wastani wa watalii laki nne kila mwaka

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na rais Dokta JAKAYA KIKWETE, imekuwa ikisisitiza mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje kuimarisha utendaji wao wa kazi kwa kuendeleza diplomasia ya kiuchumi badala ya uwakilishi wa kisiasa pekee ili kukuza uchumi wa nchi

No comments:

Post a Comment