Wednesday, February 25, 2015

Tanzania yaweka mipango ya kuwainua wafugaji nyuki

Dakta ANACLETI KASHULIZA
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi – NEEC Dakta ANACLETI KASHULIZA amesema kuwa TANZANIA imeweka malengo SITA yenye lengo la kuwainua wafugaji nyuki nchini katika maeneo ya mijini na vijijini ili waweze kuzalisha asali yenye kiwango kinachokubalika kimataifa.

Dakta KASHULIZA ameyasema hayo Jijini ARUSHA wakati wa kongamano la kwanza la ufugaji nyuki katika Bara la AFRIKA linalojumuisha wafugaji nyuki kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa Dakta KASHULIZA, TANZANIA inapaswa kuzalisha asali inayokubalika katika nchi mbalimbali Duniani hususani MAREKANI ambapo hivi sasa wananunua asali kwa wingi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa huduma za misitu nchini JUMA MGOO amesema sera na sheria za umiliki wa misitu zinaruhusu kumiliki maeneo kwa kufuata ngazi zote muhimu ambapo asilimia Arobaini ya mistu inamilikiwa na serikali na asilimia Arobaini na Tano iko chini ya usimamizi wa vijiji. 

No comments:

Post a Comment