Tuesday, February 24, 2015

Uzalishaji aina mpya ya Mgomba, wakulima wapewa darasa.

Na Ramadhani Mvungi, Arusha. 

Kituo cha utafiti na mafunzo ya kilimo cha mazao ya Mboga, Matunda na Maua cha Tengeru Arusha kikishirikiana na taasisi za TAHA na TAPP kimeanza kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu uzalishaji wa aina mpya ya zao la mgomba kupitia mashamba darasa.

Hatua hiyo ni mpango mahususi wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbogamboga, matunda na maua katika kuendeleza dhana ya kilimo biashara nchini.
 Ikiwa chini ya Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika kituo cha HORTI-TENGERU kinasema, utafiti uliofanywa umebaini aina hiyo mpya ya migomba, kuwa na kiwango cha juu cha uzalishaji wa zao la ndizi, ikiwa na uwezo wa kuvunwa migomba 1450 katika heka tofauti na ile ya awali yenye uwezo wa kuzalisha migomba 400 pekee katika kipindi cha mwaka mzima.

Mkuu wa kituo cha utafiti cha HORTI-TENGERU Juma Shekidele pamoja naye meneja uzalishaji kutoka taasisi ya TAPP kanda ya Kaskazini Milton Chitanda,wametoa mwito kwa wakulima kuzitumia teknolojia mpya zinazoibuliwa na watafiti, ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na matunda yanayoonekana kuhitajika sakoni kwa wingi.

Chama cha wakulima wa mboga na maua nchini TAHA, kupitia kwa afisa mawasiliano wake Likati Thomas kimesema lengo la kutoa fursa kwa wakulima kutembelea mashamba darasa na kujionea teknolojia mpya ni kutoa hamasa kwa wadau wa sekta hiyo hususani vijana ili waweze kujihusisha na kilimo cha Hortculture lengo likiwa ni kupunguza adha ya ukosefu wa ajira.

Uwekezaji wenye thamani ya shilingi milioni thelathini na tano unatajwa kuweka katika mashaba darasa yaliyopo eneo la Horti-Tengeru ambapo wakulima takribani mia saba wamepatiwa mafunzo ya teknolojia za usambazwaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa matone na matumizi ya mbolea

No comments:

Post a Comment