Monday, March 16, 2015

KUANDAA NA KUSAFIRISHA MAYAI YA KUKU WA KIENYEJI

Kutunza mayai kabla ya kuyasafirisha
Mayai ya kuku wa kienyeji yakiwa kwenye kiota
Ukiamua kufuga kuku wako wa asili kwa ajili ya kupata mayai ya kuuza, kumbuka kuzingatia mambo yafuatayo: -Usiyaache mayai ndani ya viota kutagia kwa muda mrefu. Yaokote mayai mara kwa mara kutegemeana na utagaji, ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai na kuku wenyewe. Mayai yasipohifadhiwa vizuri ni rahisikuharibika. Hivyo ni muhimu yahifadhiwe vyema kabla hayajapelekwa sokoni.-Fanya yafuatayo ili mayai yawe salama:  =Yatenge mayai yenye nyufa, yatumiwe nyumbani kwa kula.  =Kama yamechafuka ondoa uchafu kwa mikono mikavu. Usiyaoshe kwa majiyataharibika upesi, hutaweza kuyahiifadhi kwa muda mrefu. =Yahifadhiwe sehemu isiyokuwa na joto
Kusafirisha mayai 

Mayai yanayosafirishwa yawekwe kwenye chano (tray) za kubebea mayai na kuwekwa kwenye makasha (boksi) kwa utaratibu ufuatao:-• Mayai yapangwe kwenye chano sehemu iliyochongoka ikiwa inaangalia chini• Chano zipangwe ndani ya kasha kwa mpango unaokubalika• Kasha liwe na ukubwa unaolingana na chano kuepusha mtikitisiko• Kasha liruhusu mzunguko wa hewa• Kasha liwe imaraKama hakuna chano ndani ya mazingira yako, yapakie mayai katika chombo imara kwakuyachanganya na pumba ya mpunga au kitu chochote laini kuzuia yasivujike. 

Mayai kwenye chano (tray) tayari kwa kusafirisha

CHANZO: Rural Livelihood Development Company 

No comments:

Post a Comment