Monday, March 16, 2015

MPAPAI (Carica papaya) DAWA YA KUTIBU MAGONJWA YA MIFUGO

Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati. Matunda, majani na utomvu wake hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali ya dunia, matunda na utomvu wake umekuwa ukitumika kutengeneza bombe na waini. Mpapayi una viini hai vingi lakini hivi viwili ni muhimu kwa kutibu magonjwa na kusaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri: chymopapain and papain. Kiasi cha viini hai hivi hutofautiana kwenye matunda, utomvu, majani na mizizi lakini pia kutegemeana na umri wa mti na njia ya kutengeneza dawa yenyewe.
Matumizi kwa mifugo

-Kutibu magonjwa ya bakteria: Matawi na mbegu za mpapai vina uwezo wa kutibu magonjwa yanayoenezwa na bakteria hawa: Staphylococcus aureua, Escherichia coli, Salmonella typhi na Bacillus subtilis.-Kutibu magonjwa ya fangasi: Utomvu wa mpapai unauwezo wa kutibu fangasi inayoenezwa na Candida albicans-Magonjwa ya minyoo:Unga wa mbegu za mpapai unauwezo wa kutibu minyoo ya umbwa inayojulikana kamaDirofilaria immitis (inayoshambulia moyo). Wapewe dozi ya milligram 60 kwa kila kilo moja ya uzito wa mbwa kwa muda wa siku 30. Minyoo mingine pia inaweza kutibiwa na mmea wa mpapai kama Ascaris suum kwa nguruwe katika dozi kati ya milligram 4-8 kwa kila kilo moja ya uzito wa nguruwe kwa muda wa siku 7. Utibuji wa minyoo kwa mifugo ndiyo kivutiuo kwa wafugaji.
-Mpapai pia unauwezo wa kusaidia mnyama aharishe ili kutoa kitu ambacho hakifai tumboni.Kwa binadamu mmea huu umekuwa ukitumika sehemu mbalimbali kutibu magonwa/matatizo yafuatayo: Kuharisha na kuharisha damu, magonjwa ya figo, ini, kichaa, mafua, homa, kuongeza utoaji wa maziwa, matatizo ya mmeng’enyo wa chakula, vidonda na asthma.

No comments:

Post a Comment