Monday, March 16, 2015

ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU SIKU YA 1 HADI WIKI YA 5

UtanguliziKwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa na kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige  kuku  anavyofanya.  Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na kukosa uangalizi wa karibu.Ni lazima  vifaranga waangaliwe kwa  kuwapatia nyumba yenye joto,  chakula kinachofaa na  maji safi, kuwakinga dhidi  ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na  kuwatibu wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri  ambao hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida.Wafugaji wengi  vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga wake kwa muda mrefu hadi  wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku  kurudia kutaga na  hivyo  kupata vifaranga wachache zaidi  kwa  mwaka.  Lakini vifaranga vikiondolewa kwa  kuku  mapema, kama  majuma matano hivi baada ya kuanguliwa, na  wakatunzwa na  mfugaji,  kuku  hutaga mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji  huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi.Mwongozo huu  unaeleza jinsi ya  kufuga vifaranga vizuri  ili hatimaye mfugaji  apate faida Zaidi.
Sehemu ya KwanzaNyumba ya kulelea Vifaranga

Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufikirie yafuatayo:-a          Nyumba ya  vifaranga iwe karibu na  nyumba yako  mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.b)   Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga  mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.c)   Nyumba ya  vifaranga isiruhusu ubaridi au  unyevu au  wanyama waharibifu kuingia.Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.d)   Nyumba iwe na  eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya  kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.e)   Ijengwe kwenye sehemu  isiyoelekea upepo  unaotoka  kwenye nyumba  ya  kuku wakubwa.  Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.
Ukubwa  wa Nyumba
Endelea kusoma  HAPA kwa kubonyeza namba 6


No comments:

Post a Comment