Friday, March 27, 2015

wakulima moshi wakabiliana na ukame

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, ABDULARAMAN KINANA
Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga katika SKIMU ya umwagiliaji katika Halmashauri ya wilaya ya MOSHI, mkoani KILIMANJARO wanakabiliwa na tatizo la ukame unaosababisha upungufu wa maji na kuharibu miundombinu ya SKIMU hiyo na kuhatarisha uzalishaji wa mpunga.

Hayo yalibainika katika ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, ABDULARAMAN KINANA ambazo zilianzia katika kijiji cha MIKOCHENI hapa wilayani MOSHI mkoani KILIMANJARO kijiji kilichopo pembezoni mwa kiwanda cha Sukari cha TPC.

Ziara ya KINANA ikamfikisha katika SKIMU ya umwagiliaji ya LOWA iliyopo wilayani humo ambapo SKIMU hiyo hivi sasa haina tija tena licha ya kudumu kwa uzalishaji kwa zaidi ya miaka

Akitoa taarifa ya SKIMU hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya MOSHI, FULGENCE MPONJI amesema SKIMU hiyo yenye wakulima ELFU TATU, hivi sasa inauweza wa kulimwa Hekari 700 tu, tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya changamoto hiyo, ambapo wakulima hao walikuwa na uwezo wa kulima Hekari 1500.

No comments:

Post a Comment