Wednesday, March 25, 2015

TANZANIA na KENYA zatiliana saini kudhibiti biashara haramu ya mazao ya misitu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Maliasili nchini Kenya Richard Lusiambe (wakwanza kulia) akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki nchini Tanzania Gladness Mkamba mara baada ya kutia saini makubaliano ya Tanzania na Kenya kupiga vita biashara haramu ya mbao pamoja na mazao ya misitu inayofanyika kupitia mipaka ya nchi hizo katika mkutano uliofanyika jijini Arusha na Kuandaliwa na Shirika la kimataifa la kulinda wanyama na viumbe hai World Wildlife Foundation (WWF) ambao n
Serikali za KENYA na TANZANIA zimetiliana saini makubaliano ya kudhibiti biashara haramu ya mazao ya mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na mbao na biashara ya mkaa 


Naibu Mkurugenzi wa Misitu nchini akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira GRADNESS MKAMBA,katika zoezi hilo jijini ARUSHA ambayo yamefadhiliwa na shirika la Uhifadhi wa masingira Duniani WWF,amesema makubalianao hayo yatasaidia biashara ya misitu inafanyika kwa kufuata sheria na si kwa njia za panya. 



Mara baada ya kusaini makubaliano hayo,Naibu Mkurugenzi wa Misitu ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira GRADNESS MKAMBA amesema biasahara haramu ya mbao na mkaa imekuwa ikifanyika kwa njia za panya na sasa kupitia makubaliano hayo itadhibitiwa. 



Katibu Mkuu anayeshughulikia mazingira na maliasili nchini KENYA, Dk RICHARD LESIYAMPE,amesema misitu inafaida nyingi kiuchumi na hivyo ni vema kuwe na utaratibu sahihi. 



Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Uhifadhi wa Mazingira Duniani WWF anayewakilisha nchi ya TANZANIA,AMANI NGUSALU,amesema nchi hizo zilikuwa na maeneo makubwa ya misitu lakini kwa sasa hali ni tofauti. 



Makubaliano kama hayo yalishafanyika baina ya nchi ya TANZANIA na MSUMBIJI mwaka 2013 na yanadaiwa na wataalamu wa misitu kuonyesha mafanikio makubwa.
(IMETOLEWA NA TBC1)

1 comment: