Friday, March 27, 2015

Treni ya mizigo kutoka Bandari ya DSM - ISAKA hadi KIGALI yazinduliwa jijini DSM


Fri Mar 27 2015

 safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya Reli ya Dar es salaam aa mkutano wa nchi sita za ukanda wa kati na walipotembelea

Rais Paul Kagame wa Rwanda akipeperusha bendera kuashiria kuzinduliwa kwa safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya Reli ya Dar es salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais PAUL KAGAME wa RWANDA na RAIS JAKAYA KIKWETE wa TANZANIA wameridhia kutekelezwa kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka bandari ya DSM-ISAKA hadi KIGALI nchini RWANDA utakaozihusisha nchi tano za AFRIKA MASHARIKI baada ya kuona fursa zilizopo za kibiashara.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa nchi sita za ukanda wa kati na walipotembeleaBandari za DSM na Shirika la Reli TRL, marais hao wamesema ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ni muhimu kuweka wazi faida za mradi huo kwa kila nchi ili itambue jinsi wananchi wake watakavyofaidika kiuchumi na kijamii kabla haijatoa rasilimali zake kuijenga Reli hiyo.

Rais JAKAYA KIKWETE amemuhakikishia RAIS PAUL KAGAME wa RWANDA kuwa amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi bandarini hapo na miundombinu iliyowekezwa itaongeza kasi ya ushirikiano wa nchi za ukanda wa kati

Naye Rais PAUL KAGAME ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweza kupunguza msongamano wa mizigo bandarini na kuhakikisha mizigo inasafirishwa kwa wakati kwenda nchi jirani zinazotegemea bandari hiyo ikiwemo nchi yake ya RWANDA.
Wakati wa majadiliano wa mkutano wa jukwaa la wawekezaji ulioongozwa na RAIS PAUL KAGAME wadau wameelezea namna ya kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo ambapo sekta binafsi ndio itakayopewa jukumu hilo kwa ushirikiano na sekta ya umma.
Bandari za DSM na Shirika la Reli TRL, marais hao wamesema ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ni muhimu kuweka wazi faida za mradi huo kwa kila nchi ili itambue jinsi wananchi wake watakavyofaidika kiuchumi na kijamii kabla haijatoa rasilimali zake kuijenga Reli hiyo. Rais JAKAYA KIKWETE amemuhakikishia RAIS PAUL KAGAME wa RWANDA kuwa amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi bandarini hapo na miundombinu iliyowekezwa itaongeza kasi ya ushirikiano wa nchi za ukanda wa kati Naye Rais PAUL KAGAME ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweza kupunguza msongamano wa mizigo bandarini na kuhakikisha mizigo inasafirishwa kwa wakati kwenda nchi jirani zinazotegemea bandari hiyo ikiwemo nchi yake ya RWANDA. Wakati wa majadiliano wa mkutano wa jukwaa la wawekezaji ulioongozwa na RAIS PAUL KAGAME wadau wameelezea namna ya kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo ambapo sekta binafsi ndio itakayopewa jukumu hilo kwa ushirikiano na sekta ya umma
.

No comments:

Post a Comment