Thursday, March 26, 2015

NORWAY YADHAMIRIA KUWEKEZA LINDI KATIKA SEKTA YA GESI NA UVUVI

Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik (Katikati) akikagua baadhi ya mabwawa ya ufugaji samaki manispaa ya Lindi walipotembelea mradi wa uvuvi katika Ziara ya Mameya wa miji ya Norway waliokubali kujenga urafiki na manispaa za Lindi na Mtwara,Kushoto ni Abdilah Salum mmiliki wa mabwawa hayo na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nasor Hamid.





Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik akipokea maelezo ya hali ya Uvuvi Ndani ya manispaa ya Lindi toka mkurugenzi wa manispaa Kelvin Makonda huku mmiliki wa mabwawa hayo akielezea mipango yake ya baadae ikiwa pamoja na kuiomba Norway kumsaidia Elimu na utaalamu bora wa ufugaji wa Kisasa.
Mabwawa yanayotumika kwa ufugaji wa samaki.
Meya wa manispaa ya Alstahaug,Bard Anders Lango akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dk. Nassor Hamid wakibadilishana mawazo juu ya Ushirikiano huo ikiwemo Uwekezaji katika mji wa Lindi ambao hauna hata kiwanda kimoja hadi sasa huku kukiwa na harakati za kujengwa kwa kiwanda cha simenti cha Meis kitakachochangia ajira mbalimbali.
Meya wa manispaa ya Hammerfest Alf E Jakobsen (kati)akisikiliza maelezo ya Ufugaji wa samaki toka kwa Afisa Uvuvi wa manispaa ya Lindi Bi Sharifa Tomera.

Ujumbe toka Norway wakipata maelezo ya ukaushwaji wa samaki kwa njia ya kienyeji kutokana na kukosa dhana bora.

Na ABDULAZIZ ,Lindi
Miji miwili ya Hammerfest na Sandnessjoen iliyoko nchini Norway Imekubali kuanzisha ushirikiano baina ya manispaa ya Lindi na Mtwara Ambapo kwa pamoja wameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi pamoja na wanajamii kuwekeza katika Elimu ikiwemo kujijengea Tabia ya Kulipa kodi ambazo zitarudi katika huduma za jamii.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano baina ya viongozi wa miji hiyo na Manispaa hiyo baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Gesi na Uvuvi vitu ambavyo vinachangia pato kubwa katika Nchi zao.

Katika makubaliano hayo viongozi kutoka pande zote wamekubaliana kuwa mji wa Harmmerfest utashirikiana na Lindi na ule wa Sandnessjoen utashirikiana na Mtwara, ushirikiano ambao unalenga kuzitumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi kupitia sekta hizo ili kuhakikisha mikoa ya kusini inanufaika na rasilimali zake ikiwemo Ardhi ya kutosha na fukwe zenye ubora.

Akizungumzia umuhimu wa makampuni ya mafuta katita mji wa Sandnessjoen Meya wa mji huo Bard Anders Lango ameeleza kuwa mji wake unanufaika na mafuta na asilimia kubwa ya wananchi ni walipa kodi na asilimia 12 ya mapato urudishwa katika huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya.

Akiongea na globu hii,Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi Kelvin Makonda kwa Upande wake ametoa Shukrani kwa ujio huo na Kuanzishwa kwa ushirikiano baina ya miji hiyo na mikoa ya kusini kutasaidia kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na kuwezesha wananchi kuwa sehemu ya mafanikio ya kuanzishwa kwa miradi ya umma katika maeneo yao.

Huu ujio umekuja muda muafaka huku manispaa yangu kwa kushirikiana UTT tayari imepima Viwanja vya kutosha na tumeanza mchakato wa kuviuza na hata hawa wageni wetu tumewapa Fursa ya kununua viwanja kwa ajili ya shughuli za uwekezaji ikiwemo Hotel,Elimu na Viwanda maeneo yapo ya kutosha".

Katika ziara hiyo inayoongozwa na Balozi wa Norway nchini Tanzania,Bi Ingunn Klepsvik walitembelea Mabwawa ya Uvuvi ya ASM Trading 2005 na kumilikiwa na Abdillah Salum Mfaume ambayo tayari jumla ya Samaki 96468 wameshapandwa katika mabwawa hayo.

Aidha Bw Abdilah salum alitoa wito kwa ugeni Huo kusaidiwa utaalam wa kutosha katika Ufugaji wa Kutosha bila ya kuathiri Mazingira na kubainisha kuwa matarajio yake ni kuvuma zaidi ya kilo 25000 katika kipindi cha miezi sita ijayo hali itakayomwongezea kipato na kujiwezesha kuboresha Uvuvi katika mkoa wa Lindi

No comments:

Post a Comment