Sunday, March 22, 2015

SIDA yatoa msaada wa fedha kuendesha miradi ya kilimo


Shirika la Maendeleo la SWEDEN -SIDA limetoa EURO Milioni 2.5 kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki katika kuendeleza mradi wa uendelezaji biashara ya mazao ya kilimo hai. 


Mradi huo ambao utachukua takribani miaka minne 2015/2019 utazishirikisha nchi zote tano za Afrika Mashariki 

Akizungumzia mradi huo mjini Unguja,Mtendaji Mkuu wa Uendelezaji wa kilimo hai Tanzania JORDAN GAMA amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wakulima na wasindikaji wa kuzingatia ubora wa kuzalisha mazao ya kilimo hai.

No comments:

Post a Comment