WAJASIRIAMALI WAPATA MAFUNZO USINDIKAJI MUHOGO
WAJASIRIAMALI 16 kutoka Mikoa ya Mwanza, Pwani na Kagera wamepata elimu
ya usindikaji wa zao la muhogo na viwango vinavyozingatia ubora unaokubalika
katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EA C).
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, wilayani Misungwi baada ya
mafunzo hayo, mshauri wa usindikaji na masoko wa IITA Dkt. Gabriel Nduguru,
alisema wakulima wasindikaji wa zao la muhogo, hawakuwa na elimu ya kutosha
kuhusu viwango na ubora wa bidhaa zao.
Alisema kuwa mafunzo hayo kwa wasindikaji hao, yalitolewa na Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango
nchini (TBS ).
Alisema IITA ilifanya utafiti na kubaini changamoto hiyo kwa wasindikaji wengi
wa zao la muhogo, hivyo ikaamua kutoa elimu inayohusu ubora na viwango kwa
wasindikaji hao ili kuwawezesha kupata masoko ya uhakika.
"Wakulima na wasindikaji hao hawakuwa na elimu, hivyo bidhaa zao hazikuwa
bora na salama na zilitishia afya za walaji.Baada ya kubaini hilo tukaona
tuwafundishe jinsi ya kusindika muhogo salama kwa kuzingatia viwango vya ubora
kulingana na mahitaji ya walaji," alisema Dkt. Ndunguru.
Alisema wanafanya utafiti wa mazao na kusaidia kuainisha viwango vinavyotumika
kwa nchi za EAC, baada ya kuridhiwa na mawaziri wa nchi za Jumuiya hiyo.
Alisema wananchi watafahamu viwango vya ubora baada ya kuwapa mafunzo ya
usindikaji na watazalisha chakula chenye ubora na kuuza katika masoko ya
uhakika na watajiongezea kipato .
Dkt. Ndunguru alisema changamoto kubwa kwa wasindikaji zao la muhogo, ni
vifungashio na mitambo ya kisasa kwani ni kiwanda kimoja tu ambacho
hakitoshelezi mahitaji.
No comments:
Post a Comment