ALLIANCE GINNERIES LTD WASHAURI SERIKALI ITOE ELIMU UBORA WA MBEGU MPYA
UONGOZI wa
kinu cha kuchambua zao la Pamba cha Alliance Ginneries Ltd, Wilayani Bariadi,
Simiyu umeishauri Serikali itoe elimu kuhusu ubora wa mbegu mpya ya UKM08 ili
kuondoa mkanganyiko kwa wakulima na kuiondoa sokoni mbegu ya UK91 ili
kuimarisha na kuboresha kilimo cha mkataba.
Pia kampuni
hiyo imewekeza kwa kusambaza tani 20,000 za mbegu hiyo aina ya UKM08 kwa
wakulima wa mashamba darasa, katika vijiji vya Ikungulyabeshi, Nguliati,
Kilalo, Ikungulyabashashi na Nyamagana, Kata ya Kasoli.
Ushauri huo
ulitolewa juzi na meneja wa kinu hicho cha Alliance, Boaz Ogola, alipozungumza
na waandishi wa habari, waliotembelea mashamba darasa yanayosimamiwa na kinu
hicho mkoani Simiyu, baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa zao la pamba
(Ginners) wa Wilaya za Bariadi na Itilima, kuhusiana na kilimo cha mkataba na
changamoto zake.
Alisema mbegu ya UK91 ambayo imedumu sokoni
kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10 imechoka, hivyo kusababisha wadudu waizoee na
kuishambulia kwa urahisi, ambapo aliwataka wakulima kuacha kuitumia na
kuendelea nayo ni kuzidi kujididiza kiuchumi.
Ogola
alisema madai ya baadhi ya wakulima na wanasiasa kuwa mbegu hizo za UKM08
zisizo na manyoya hazioti ni uongo uliopitiliza, bali zimeonesha kuwa na tija
kwa wakulima tofauti na mbegu ya UK91 ambayo uzalishaji wake kwa ekari ni kilo
200 hadi 300.
"Kitaalamu
ili pamba iwe na tija kwa mkulima, mbegu isikae sokoni kwa miaka 10, inachoka
na wadudu wanaizoea, hivyo nguvu ya uzalishaji inapungua. UK 91 imechoka sasa
inapaswa iondoke badala yake wakulima watumie UKM08 ambayo imeonyesha tija na
ina uwezo wa kuzalisha kilo 800 hadi 1,200 kwa ekari,"alisema Ogola na
kuongeza;
"Uwekezaji
huo wa tani 20,000 za mbegu za UKM08 kwa wakulima tulioingia nao mkataba,
tunaamini baada ya miaka miwili tani milioni 1,440,000 zitakuwa zimezalishwa
mbegu za kutosheleza mahitaji ya wakulima," alisema.
Alisema
mbegu hizo zina tija kwa pande zote kwa mkulima na mchambuaji endapo zitapandwa
na kutunzwa kitaalamu na baada ya kuvuna na kuchambuliwa pamba hiyo mbegu bora
zitapatikana kwa asilimia 75.
Alidai
kwamba baada ya kuchambuliwa kwa pamba uzalishaji wa nyuzi ni asilimia 33,
mbegu asilimia 63 na asilimia 2 ni taka (west) kulinganisha na mbegu ya UK91.
Hivyo serikali haina budi kuiondoa mbegu ya UK91 sokoni ili wakulima watumie
UKMO8 ambayo ina tija kwao na yenye uwezo wa kuzalisha kilo 800 hadi 1,200 kwa
ekari.
Aidha
mratibu wa Mpango wa Kuendeleza Kilimo cha zao la Pamba na Viwanda vya nyuzi
(CDTP), Donald Sayi, aliwataka wawekezaji wa zao hilo kutokana na uzalishaji
wake kushuka waangalie na kuwekeza kwenye maeneo wanayoweza kupata faida.
Alisema
wakulima wanawategemea wawekezaji hao ambao ni wanunuzi na wachambuzi, hivyo
mapato yao yakiimarika, halmashauri pia zitapata mapato mazuri na kuzishauri
zitenge asilimia 10 ya mapato hayo kwa ajili ya elimu ya huduma za ugani kwa
wakulima.
"CDTP hatuna nia ya kumweka mtu pembeni, tunataka twende sote kwani
mafanikio ni yetu wote. Wakulima wapate faida kwa jasho lao kadhalika na
wachambuzi pia. Kipato kikiimarika kati ya wakulima na wachambuzi ni faraja
kwetu,"alisema Sayi.
Alisema
kilimo cha mkataba cha zao la pamba kinafadhiliwa na Tanzania Gatsby Trust
(TGT), ambapo CDTP ni washauri, lakini baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakikipinga
kwa madai kuwa wanunuzi na wachambuaji wa zao hilo wanawanyonya wakulima kwa
kuwakopesha pembejeo, mbegu na viuadudu, jambo ambalo si kweli.
Good Blog with good Pictures, i really like it.We provides
ReplyDeleteTempo traveller rental gurgaon
Tempo traveller rental noida
Tempo traveller hire
Tempo traveller
Tempo traveller for outstation
Tempo traveller rent in bangalore
Tempo traveller rental in gurgaon
Tempo traveller hire in faridabad
innova taxi rental faridabad
Innova taxi rental in faridabad
Innova taxi rental in gurgaon
Innova taxi rental in noida
Innova taxi rental in delhi
Innova taxi rental in ghaziabad
Innova taxi rental in ballabgarh
Innova taxi rental for airport
Innova taxi rental for outstation
Hire innova taxi
Rent innova taxi
for easy travel call us +91-9560075009