Ripoti ya Benki hiyo
imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi
nzuri ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa
kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni 202 kujikwamua
katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta
mafanikio kwa jumla.
Ripoti hiyo inayoitwa
“Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,” inaeleza
kuwa nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la
uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha taratibu za
usimamizi na umiliki wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika, Ripoti
hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia
47.5 ya watu wake wana kipato chini ya dola za Marekani $1.25 kwa
siku..
“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,” anasema Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
“Kuboresha usimamiaji wa
ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi zaidi kwa
waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao
wanakwazwa kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na
lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.”
Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Hata hivyo kumekuwa na
matumaini ya maboresho chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi
za Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo
mpango wa kutumia ardhi kwa mafanikio ya pamoja unaweza kuleta mapinduzi
ya uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na kuondoa umaskini wa
kutupea Afrika..
Mpango wa kuleta mabadiliko
Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake katika kipindi cha muongo ujao kwa::
· Kuwa na mabadiliko na uwekezaji kurasimisha ardhi na maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi. Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa na kujengwa bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya watu asilimila 60 barani Afrika.

Kukabiliana na udhaifu wa
utawala na rushwa katika mfumo wa usimamizi wa ardhi katika nchi za
Afrika ambao kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya
wananchi walio maskini. Serikali za Afrika kuwa na dhamira ya
kisiasa kuhimiza mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na
uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .
Ripoti hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu nchi za Afrika na washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha dola za Marekani bilioni 4.5 katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji

No comments:
Post a Comment