Friday, March 7, 2014

BENKI YA AFRICA KUTOA MIKOPO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NCHINI




Benki ya Africa (Boa) imesaini mkataba wa Sh. bilioni 15 na European Investment Bank kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wakati nchini ili kuinua biashara zao.

Mkataba huo ulisainiwa juzi jijini Dar es Salaam na viongozi wa Boa Tanzania na Balozi wa European Investment Bank, Filberto Ceriani, sasa wafanyabiashara sasa ni wakati wao kwenda BOA benki kwaajili ya kujipatia mkopo wako katika kuongeza ufanisi wa biashara yako.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Afisa Mwandamizi wa European Investment Bank, Pim Van Ballekom na  Mkurugenzi wa Boa, Ammish Owusu Amoah walisema zimetolewa Euro milioni saba  sawa na Sh, bilioni 15 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati wa hapa nchini.

Walisema wameamua kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wafabiashara wadogo na wakati kuendeleza biashara zao na hivyo kujikwamua kimaisha, pia walisema  kuwa, mikopo hiyo itatolewa kwa kuzingatia kigezo cha biashara ya mtu anayeomba na wanaanzia Sh. milioni 25 ambazo zinatakiwa kurudishwa kwa wakati muafaka ambao umepangwa na benki hiyo.

Walisema benki ya Boa ilianza muda mrefu kutoa mikopo hiyo na na kwamba fedha hizo kutoka European Bank ni nyongeza na kuahidi watatoa mikopo hiyo ili wafanyabiashara wanufaike nayo katika biashara zao.

Amoah alisema wamefurahi kuona European Bank wanatambua mchango wao na kuamua kuwaongeza fedha za kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati ambao wengi wao wanafanya biashara bila ya kujua mikopo yao wanaipata wapi.

Alisema vigezo vitakavyotumika kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo ni pamoja na muombaji kuonyesha biashara yake ambayo itakaguliwa ili uweze kupatiwa mkopo kwa ajili ya kuiendeleza. - See more at: http://ajirazetu.com/blog/227-benki-ya-africa-kutoa-mikopo-kwa-wafanyabiashara-wadogo-nchini.

No comments:

Post a Comment