Serikali
ya Kenya tarehe 13 ilifanya mkutano wa baraza la mawaziri ikiidhinisha
kuanzisha eneo la kwanza la biashara huria mjini Mombasa.
Mkutano
huo ulioongozwa na rais Uhuru Kenyatta. Sababu ya kuidhinisha kuanzisha eneo la
biashara huria ni kwamba serikali ya Kenya imetambua kuwa uchumi wa dunia
unafufuka, na uchumi wa nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara una
mwelekeo mzuri, na mambo hayo yote yameonesha mustakabali mzuri wa uchumi wa
Kenya.
Mji wa
Mombasa ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya, ni bandari kubwa zaidi nchini
humo, pia ni kituo muhimu cha viwanda na biashara. Mji huo umeunganishwa na mji
mkuu Nairobi kwa reli, barabara kuu na mabomba ya kusafirisha mafuta. Bandari
ya Mombasa ina vifaa vya kisasa, ambayo inashughulikia uchukuzi wa baadhi ya bidhaa
za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda. Bandari hii iko katikati ya
pwani ya Afrika Mashariki. Hakuna bandari kubwa kaskazini yake hadi bahari
nyekundu, na kusini yake kuna bandari ya Durban ya Afrika Kusini tu ambayo ina
uwezo wa kushindana na bandari hii. Sababu zote hizi zimeweka mazingira mazuri
ya kuanzisha eneo la kwanza la biashara huria mjini Mombasa.
Licha ya
Mombasa, serikali ya Kenya pia inapanga kuanzisha maeneo ya biashara huria
katika miji ya Kisumu na Lamu. Hivi sasa imetenga ardhi kilomita 3,400 za mraba
kwa ajili ya ujenzi wa maeneo ya biashara huria. Eneo la biashara huria la
Mombasa litakuwa kilomita elfu 2000 za mraba, lile la Kisumu na lile la Lamu
yote ni kilomita 700 za mraba.
Taarifa
zilizotolewa na serikali ya Kenya zinaonesha kuwa, ushuru wa bidhaa utafutwa
katika maeneo hayo ya biashara huria, na hatua hii itaimarisha na kuboresha
biashara kati ya nchi za Afrika Mashariki, ya Kati na Kusini. Pia Kenya
inatazamiwa kuagiza bidhaa za nchi hizi moja kwa moja katika maeneo ya biashara
huria badala ya kwenda Umoja wa Falme za Kiarabu, China na Japan.
No comments:
Post a Comment