Ufugaji
wa nyuki unaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato cha ziada kwa wakulima wadogo
wadogo.
Uzalishaji
wa asali nchini Tanzania umekuwa ukitegemea sana wafugaji wadogo wadogo,
wanaotumia njia za kiasili kama vile mizinga ya magogo au vyungu, kwa nyuki wa
kiafrika ambao ni wengi sana kwenye mapori.
Ni muhimu kuwa na utaalamu wa kufuga nyuki
Mkulima
ambae anahitaji kufuga nyuki ni lazima awe na uelewa wa mzunguko wa maisha ya
nyuki. Anaye anza ni lazima aulize wafugaji wenzake ambao wana uzoefu wa
kutosha, au kujiunga katika kikundi cha ufugaji ili apate ufahamu zaidi juu ya
ufugaji wa nyuki.
Tafuta
sehemu salama kwa ajili ya mzinga
Ni vizuri
kutafuta mahali pazuri, salama, na penye sifa ya kufugia nyuki. Vifaa vyote
vikishapatikana jambo linalofuata ni kuchagua mahali gani pa kuweka mzinga. Ni
vizuri sehemu hii ikawa mahali ambapo makundi ya nyuki hukusanyika mara kwa
mara.
Ni wapi
pa kuweka mzinga!
Mara
nyingine kupata eneo sahihi ni tatizo. Ni vizuri kuzingatia yafuatayo:
•
Kulingana na hali ya kujilinda ya nyuki wa Afrika, haishauriwi kuweka mzinga
shambani au karibu na shamba (weka umbali wa mita 150-200 kutoka kwenye mazao
au nyumbani)
• Mzinga
ni lazima uwekwe sehemu ambayo haitasababisha upotevu wa nyuki wanaporudi
kutoka nje ya mzinga (wasiingie kwenye kundi lisilokuwa lao)
• Mizinga
isiwekwe mbalimbali sana ili kuepusha usumbufu wa kutembea mbali kwa mfugaji
wakati anapokagua. Eneo la kuweka mizinga ni lazima liwe :
• Kimya
na mbali ya jumuia (hospitali, shule, na viwanja vya michezo) na maeneo ya
biashara au viwanda.
• Karibu
na maji masafi-kandokando ya mto, mabwawa ya samaki, mabeseni ya maji au sehemu
ya matone.
• Iwe
karibu na chakula cha nyukimimea inayochanua, miparachichi,
nazi,
euculptus, migunga n.k
• Iwe
sehemu ambayo ni kavu na isiwe sehemu ya tindiga kwani unyevu unyevu
husababisha ugonjwa wa ukungu (fungal disease) na pia huzuia utengenezaji mzuri
wa asali.
• Iwe
mbali na watu waharibifu na iliyojificha kuepuka waharibifu.
• Sehemu
ya mizinga ni lazima iwe inafikika kirahisi kwa kipindi chote cha mwaka ili iwe
rahisi kuhamisha nyuki pale inapohitajika.
• Kuwe na
kivuli cha kutosha hasa wakati wa mchana jua linapokuwa kali, na kusiwe na
upepo mkali.
• Iwe
mbali na mashamba, ambapo dawa za kuulia wadudu zinatumika.
Vichaka
au wigo unaotenganisha mizinga na kuzuia wavamizi ni muhimu ili kupunguza ukali
wa nyuki.
Jinsi ya
kuweka mzinga
Baada ya
sehemu ya kuweka mizinga kupatikana, kinachofuata ni kuandaa mizinga kwa ajili
ya kuweka panapotakiwa.
• Safisha
mzinga kuondoa uchafu wote, utando wa buibui na aina nyingine za wadudu.
• Weka
chambo kwenye mzinga (waf ugaji wa nyuki mara nyingi hutumia nta) kwa kuipaka
katika kuta za mzinga kwa ndani.
• Mzi nga
unaweza kutundikwa kwenye mti, kwenye nguzo, kuweka kwenye jukwaa au kwenye
miamba. Hii inategemea mkulima mwenyewe anapendelea njia ipi.
Aina za
mizinga ya nyuki
Kifuniko
juu (Top bar)
Hii ni
aina ya mizinga inayotumika sana. Gharama yake ni karibi shilingi elfu hamsini
za kitanzania. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni
wa gharama nafuu. Hata hivyo mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga
mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.
Faida
• Ni
rahisi kukagua asali iliyo tayari.
• Ni
rahisi kuvuna asali kuliko kuvuna toka kwenye mzinga wa kienyeji.
• Ni
rahisi kuwatunza nyuki wakati wa kiangazi na inapokuwa hakuna maua. Mfugaji
anaweza kuwapatia nyuki chakula ili kuongeza uzalishaji wa asali.
• Kurina
asali ni rahisi sana ukilinganisha na mizinga ya magogo inayotundikwa juu ya
mti, kwa kuwa haihitaji vifaa maalumu.
• Aina
hii ya mizinga huwekwa kwa kuninginia jambo ambalo siyo rahisi kushambuliwa na
wadudu/wanyama wanaokula asali. Inajaa haraka sana wakati ambao ni msimu wa
asali kutengenezwa kwa wingi.
Hasara
• Kichane
kwenye mzinga wa boksi hakina kishikizo hivyo huvunjika kwa urahisi sana kama
hakitashikwa kwa uangalifu.
• Masega
huvunwa pamoja na asali, jambo linalolazimu nyuki kutengeneza tena masega
mengine na husababisha kupungua kwa uzalishaji wa asali.
Mzinga wa
Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi
Hii ni
aina nzuri na rahisa sana ya mzinga. Pia hufahamika kama mzinga wa fremu, kwa
kuwa ina fremu ambazo vichane vya masega hujishikiza. Pia una chumba kikubwa
ambacho malkia hutagia mayai. Malkia anazuiliwa kuhama kwenda chumba kingine
kwa kutumia waya. Kwenye chemba maalumu ya kutagia juu yake pana chemba ya
kuhifadhia asali. Vichane vya masega vinatengezwa kwenye fremu na si kwenye
nguzo kama ilivyo kwenye Top bar.
Ili
kuvuna asali, mfugaji akiwa na masega yaliyojaa asali, hutumia vifaa maalum kwa
ajili ya urinaji na kuhifadhi asali bila kupata tabu.
Langstroth
ni gali kiasi fulani kwani huuzwa kuanzia kiasi cha TSh 70,000. Unaweza kuipata
kutoka katika taasisi zilizopo hapo chini, taasisi na karakana binafsi, au
wakala wa Serikali.
Chanzo:
Mkulima Mbunifu
No comments:
Post a Comment