Muungano wa nchi
za Ulaya, EU na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, pamoja na serikali ya
Zimbabwe, zimezindua programu ya kina ya kuwasaidia wakulima maskini
wanaojishughulisha na uzalishaji mdogomdogo kuoengeza uzalishaji wao.
Programu hiyo pia inalenga kuwawezesha kushiriki
katika kilimo cha biashara kupitia mbinu jumuishi za ukulima.
Programu hiyo ya miaka minne yenye thamani ya dola
milioni 19, itasimamiwa na FAO, na itaangazia unyunyizaji maji kwa mashamba ya
wakulima wadogowadogo na shughuli za ufugaji.
No comments:
Post a Comment