Msukumo
wa uhitaji mkubwa wa parachichi kwa wingi na zenye ubora unawasukuma wakulima
kutumia teknolojia mpya.
Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea
mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una
ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora
zaidi. Utaratibu wa kupandikiza hivi sasa umekuwa silaha ya wakulima kuwakomboa
dhidi ya wadudu pamoja na magonjwa, na hili kwa sasa halifanyiki tena maabara
kama ilivyokuwa awali na hii inadhibitishwa na yale tuliyojionea Njombe
tulipotembelea wakulima.
Kwenye shamba la bwana Bosco
Kidenya, ana kitalu chenye zaidi ya miche 1200 ya miparachichi, baadhi ikiwa
tayari imeshapandikizwa na mingine ikiwa inasubiri kufikia wakati wa
kupandikiza. Huyu ni mmoja kati ya wakulima walio wengi wanaofanya kazi
kwa karibu na CARITAS Njombe, kuboresha uzalishaji wa parachichi, pamoja na
kuboresha kipato cha wakulima ambao wanazalisha matunda na mboga mboga.
Mbinu wanayotumia
Wakulima hukusanya kokwa za
parachichi kutoka maeneo ya sokoni; wanachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu
hiyo ni safi, haijaathiriwa na magonjwa na itaota. Baada ya hapo huchagua zile
zenye muundo mzuri na kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya kitalu. Baada
ya kuota huziotesha kwenye makopo, au kwenye viriba kisha kuendelea kumwagilia
maji mpaka zinapokuwa na umbo usawa wa penseli. Upandikizaji ni lazima ufanyike
wakati mmea umefikisha unene wa penseli. Kupandikiza kwa kutumia chipukizi
lililolingana na mche unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.
Upandikizaji ni lazima ufanyike
wakati ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza
ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo
liwiane na mti linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi
kukauka.
Mapandikizi ni lazima yatokane na
aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile hass, fuerte au puebla.
Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani mapya. wana mkataba na Africado,
watahitajikupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya hass. Hii ina maanisha kuwa
mkulima anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande
walau miti 5 ya parachichi aina ya hass ili kupata mapandikizi.
Njia ya kupandikiza ina ufanisi
zaidi na ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini
ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili
magonjwa. Wakulima pia wamekuwa na rikodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana
na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.
Wakulima ambao wanafanya kazi zao
chini ya CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza,
wameamua kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye vitalu
vyao. Hii ni mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima, huku akiwa
amewekeza kwa kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu na magonjwa na
kuepuka kuwa na mazao yenye ubora wa chini.
NAMNA YA KUPANDA
• Nafasi halisi inayohitajika na mmea wa
parachichi ili ukae vizuri ni nafasi ya 9m x 9m. Chimba shimo katika vipimo
vya 60sm x 60sm kwa 60sm kwenda chini kisha tenga udongo wa juu na wa
chini. Changanya udongo wa juu na mbolea ndoo moja iliyooza vizuri,
pamoja na kiganja kilichojaa cha mbolea ya minjingu.
• Ondoa mche wako kwenye kiriba ulipopandwa.
Hii itakuwa rahisi zaidi endapo ulikuwa umenyweshea muda kidogo
uliopita. Panda kwa kutumia udongo wa juu uliochanganya na mbolea
na uweke mpaka kujaza shimo.
• Mwagilia maji mara baada ya kupanda. Funika
mmea mchanga kwa kutumia majani ya migomba au aina nyingine ya
majani yanayofanana na hayo, mpaka kufikia kipindi ambacho mmea utatoa
majani mapya.
No comments:
Post a Comment