Thursday, March 13, 2014

WALIMA KOROSHO WAPATA HASARA



Mtwara. Asilimia 70 ya wakulima wa korosho wa mikoa ya Ruvuma na Pwani katika msimu uliopita wamepata hasara baada ya kuuza korosho zao chini ya Sh1,000, wakati wakulima wenzao wa Mikoa ya Tanga,Lindi na Mtwara wamepata faida kwa kuuza bei ya kati ya Sh1000 hadi Sh1,350.
 
Akizungumza na waandishi mwishoni mwa wiki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mudhihir Mudhihir alibainisha kuwa, wakulima wa mikoa hiyo wamepata hasara kwa kuuza kwa bei kati ya Sh700 hadi Sh900 chini ya bei kutokana na kutotekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani.

Alisema kutokana na sababu zikiwamo vyama vya ushirika kukosa sifa ya kukopeshwa na benki, mikoa hiyo ilishindwa kuuza korosho zao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani hali iliyotoa mwanya kwa walanguzi.

No comments:

Post a Comment