Friday, March 14, 2014

WAKAZI KUNUFAIKA NA ZAO LA TUMBAKU



WATANZANIA wa naoishi eneo la makazi ya wakimbizi la Ulyankulu, wataanza kunufaika na ushuru wazao la tumbaku ambao walikuwa hawaupati baada ya kuvunjwa kwa Kata zilizokuwa ndani ya eneo hilo. 

Akizungum zana wananchi hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua , John Kadutu, alisema utaratibu unafanywa ili nao waanze kunufaika na ushuru wa zao hilo. 

"Hivi punde wananchi wanaolima zao la tumbaku wataanza kunufaika na ushuru na hii itasaidia kusukuma maendeleo  yao mbele," alisema.

Kadutu alisema kuwa vilevile wanachangia Halmashauri kupata mapato kupitia ushuru huo unaorudishwa kwenye kata kwa ajili ya maendeleo.

Kadutu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ichemba, alisema wananchi wa eneo hilo wanalima sana zao hilo na ni jambo zuri nao kupata ushuru wa zao hilo kwa ajili ya maendeleo ya eneo lao baada ya kuikosa kwa muda mrefu sasa.

Kwa mujibu wa Kadutu ushuru wa tumbaku uliokuwa ukitolewa kwenye kata zilizokuwa ndani ya eneo la makazi ya wakimbizi, umekuwa ukipatiwa Kata zilizo jirani na eneo hilo ambalo baada ya kuvunjwa kwa Kata zake limekuwa halina wawakilishi katika Baraza la Madiwani. 

Zaidi ya wakimbizi 50,000 wanaoishi eneo hilo ambapo wengi wao tayari wamepatiwa uraia wa Tanzania baada ya kuomba na hivyo kuendelea kuishi na Watanzania wengine wanaofanyakazi kuwahudumia ikiwemo shuleni na katika zahanati.

No comments:

Post a Comment