Monday, October 15, 2012

KAZI YA MAVUNO



 
 



                                                     MW JK Nyerere akihamasisha juu ya kilimo
                                                                      na kujitegemea 

 











 

 

Sekta Binafsi Yatakiwa Kushirikiana na Serikali katika Kuendeleza Kilimo

Makamu wa raisi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Gharib Bilal amewataka wakulima kushirikiana na Serikali pamoja na sekta binafsi na kutumia rasilimali zilizopo ili kuharakisha mapindizi ya kijani.
Dkt Bilal aliyasema hayo hivi karibuni katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nane Nane yaliyofanyika mwaka huu katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Alifafanua kuwa Serikali kupitia mpango wa kukuza kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) imezamilia kuvutia uwekezaji huo wa sekta binafsi katika kilimo.
Aidha, alisema serikali tayari imeanza kuuandaa mpango wa Awamu ya pili wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo utakaojulikana kama ASDPII.
Hatua hiyo imekuja baada ya awamu ya kwanza ya programu ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini iliyoanza mwaka 2006 kufikia kikomo mwezi juni 2013.
Aliongeza kuwa katika hatua nyingine serikali kupitia programu kabambe ya kuendeleza kilimo barani Afrika (Comprehesive Africa Agricultural Development Programme-CAADP) pia imezamilia kuongeza ushirikishwaji huo wa sekta binafsi.
Dkt Bilal aliwahamasisha wawekezaji kutoka sekta binafsi kujitokeza kwa wingi ili kuongeza nguvu za serikali katika kufika lengo la Mapinduzi ya Kijani.

Sunday, October 14, 2012

MIKUMI NATIONAL PARK


Tazama mbuga zetu za Tanzania ambazo zina vivutio vizuri ambapo watu wengi hawapati nafasi 
ya kwenda kutembelea mbuga zetu.