Friday, March 27, 2015

wakulima moshi wakabiliana na ukame

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, ABDULARAMAN KINANA
Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga katika SKIMU ya umwagiliaji katika Halmashauri ya wilaya ya MOSHI, mkoani KILIMANJARO wanakabiliwa na tatizo la ukame unaosababisha upungufu wa maji na kuharibu miundombinu ya SKIMU hiyo na kuhatarisha uzalishaji wa mpunga.

Hayo yalibainika katika ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, ABDULARAMAN KINANA ambazo zilianzia katika kijiji cha MIKOCHENI hapa wilayani MOSHI mkoani KILIMANJARO kijiji kilichopo pembezoni mwa kiwanda cha Sukari cha TPC.

Ziara ya KINANA ikamfikisha katika SKIMU ya umwagiliaji ya LOWA iliyopo wilayani humo ambapo SKIMU hiyo hivi sasa haina tija tena licha ya kudumu kwa uzalishaji kwa zaidi ya miaka

Akitoa taarifa ya SKIMU hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya MOSHI, FULGENCE MPONJI amesema SKIMU hiyo yenye wakulima ELFU TATU, hivi sasa inauweza wa kulimwa Hekari 700 tu, tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya changamoto hiyo, ambapo wakulima hao walikuwa na uwezo wa kulima Hekari 1500.

Treni ya mizigo kutoka Bandari ya DSM - ISAKA hadi KIGALI yazinduliwa jijini DSM


Fri Mar 27 2015

 safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya Reli ya Dar es salaam aa mkutano wa nchi sita za ukanda wa kati na walipotembelea

Rais Paul Kagame wa Rwanda akipeperusha bendera kuashiria kuzinduliwa kwa safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya Reli ya Dar es salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais PAUL KAGAME wa RWANDA na RAIS JAKAYA KIKWETE wa TANZANIA wameridhia kutekelezwa kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka bandari ya DSM-ISAKA hadi KIGALI nchini RWANDA utakaozihusisha nchi tano za AFRIKA MASHARIKI baada ya kuona fursa zilizopo za kibiashara.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa nchi sita za ukanda wa kati na walipotembeleaBandari za DSM na Shirika la Reli TRL, marais hao wamesema ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ni muhimu kuweka wazi faida za mradi huo kwa kila nchi ili itambue jinsi wananchi wake watakavyofaidika kiuchumi na kijamii kabla haijatoa rasilimali zake kuijenga Reli hiyo.

Rais JAKAYA KIKWETE amemuhakikishia RAIS PAUL KAGAME wa RWANDA kuwa amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi bandarini hapo na miundombinu iliyowekezwa itaongeza kasi ya ushirikiano wa nchi za ukanda wa kati

Naye Rais PAUL KAGAME ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweza kupunguza msongamano wa mizigo bandarini na kuhakikisha mizigo inasafirishwa kwa wakati kwenda nchi jirani zinazotegemea bandari hiyo ikiwemo nchi yake ya RWANDA.
Wakati wa majadiliano wa mkutano wa jukwaa la wawekezaji ulioongozwa na RAIS PAUL KAGAME wadau wameelezea namna ya kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo ambapo sekta binafsi ndio itakayopewa jukumu hilo kwa ushirikiano na sekta ya umma.
Bandari za DSM na Shirika la Reli TRL, marais hao wamesema ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ni muhimu kuweka wazi faida za mradi huo kwa kila nchi ili itambue jinsi wananchi wake watakavyofaidika kiuchumi na kijamii kabla haijatoa rasilimali zake kuijenga Reli hiyo. Rais JAKAYA KIKWETE amemuhakikishia RAIS PAUL KAGAME wa RWANDA kuwa amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi bandarini hapo na miundombinu iliyowekezwa itaongeza kasi ya ushirikiano wa nchi za ukanda wa kati Naye Rais PAUL KAGAME ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweza kupunguza msongamano wa mizigo bandarini na kuhakikisha mizigo inasafirishwa kwa wakati kwenda nchi jirani zinazotegemea bandari hiyo ikiwemo nchi yake ya RWANDA. Wakati wa majadiliano wa mkutano wa jukwaa la wawekezaji ulioongozwa na RAIS PAUL KAGAME wadau wameelezea namna ya kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo ambapo sekta binafsi ndio itakayopewa jukumu hilo kwa ushirikiano na sekta ya umma

Thursday, March 26, 2015

KILIMO CHA CHA UMWAGILIAJI CHA FANIKIKIWA MKOANI ARUSHA

Skimu ya Maji ya Kabambe iliyojengwa katika Wilaya ya Monduli kata ya Majengo kuwasaidia wakulima kupata maji kwa ajili ya kilimo cha Mahindi, Ndizi na Mbogamboga, ikiwa ni sehemu ya miradi inayoratibiwa na ASDP na kusimamiwa na wadau wa maendeleo IFAD .
Mojawapo ya Shamba la Nyanya linalotumia Skimu ya Maji ya Kabambe inayoratibiwa na Miradi ya ASDP katika Wilaya ya Monduli.  
Shamba la Mbogamboga la Wakulima wa Monduli wanaotumia Skimu ya Maji ya Kabambe ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya miradi ya ASDP inayosimamiwa na wadau wa maendeleo IFAD

KILIMO CHA UMWAGILIAJI MJINI DODOMA


 Kilimo cha umwagiliaji mjini dodoma kwenye maonesho ya nanenane zikionekana mbogamboga zinavyo kubari kilimo hicho katika maonesho
 Ni zao la sukuma wiki linavyo onekana pichani katika kilima cha umwagiliaji katika maonesho ya nanenane mjini dodoma 

NORWAY YADHAMIRIA KUWEKEZA LINDI KATIKA SEKTA YA GESI NA UVUVI

Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik (Katikati) akikagua baadhi ya mabwawa ya ufugaji samaki manispaa ya Lindi walipotembelea mradi wa uvuvi katika Ziara ya Mameya wa miji ya Norway waliokubali kujenga urafiki na manispaa za Lindi na Mtwara,Kushoto ni Abdilah Salum mmiliki wa mabwawa hayo na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nasor Hamid.





Balozi wa Norway Nchini,Bi Ingunn Klepsvik akipokea maelezo ya hali ya Uvuvi Ndani ya manispaa ya Lindi toka mkurugenzi wa manispaa Kelvin Makonda huku mmiliki wa mabwawa hayo akielezea mipango yake ya baadae ikiwa pamoja na kuiomba Norway kumsaidia Elimu na utaalamu bora wa ufugaji wa Kisasa.
Mabwawa yanayotumika kwa ufugaji wa samaki.
Meya wa manispaa ya Alstahaug,Bard Anders Lango akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dk. Nassor Hamid wakibadilishana mawazo juu ya Ushirikiano huo ikiwemo Uwekezaji katika mji wa Lindi ambao hauna hata kiwanda kimoja hadi sasa huku kukiwa na harakati za kujengwa kwa kiwanda cha simenti cha Meis kitakachochangia ajira mbalimbali.
Meya wa manispaa ya Hammerfest Alf E Jakobsen (kati)akisikiliza maelezo ya Ufugaji wa samaki toka kwa Afisa Uvuvi wa manispaa ya Lindi Bi Sharifa Tomera.

Ujumbe toka Norway wakipata maelezo ya ukaushwaji wa samaki kwa njia ya kienyeji kutokana na kukosa dhana bora.

Na ABDULAZIZ ,Lindi
Miji miwili ya Hammerfest na Sandnessjoen iliyoko nchini Norway Imekubali kuanzisha ushirikiano baina ya manispaa ya Lindi na Mtwara Ambapo kwa pamoja wameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi pamoja na wanajamii kuwekeza katika Elimu ikiwemo kujijengea Tabia ya Kulipa kodi ambazo zitarudi katika huduma za jamii.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano baina ya viongozi wa miji hiyo na Manispaa hiyo baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Gesi na Uvuvi vitu ambavyo vinachangia pato kubwa katika Nchi zao.

Katika makubaliano hayo viongozi kutoka pande zote wamekubaliana kuwa mji wa Harmmerfest utashirikiana na Lindi na ule wa Sandnessjoen utashirikiana na Mtwara, ushirikiano ambao unalenga kuzitumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi kupitia sekta hizo ili kuhakikisha mikoa ya kusini inanufaika na rasilimali zake ikiwemo Ardhi ya kutosha na fukwe zenye ubora.

Akizungumzia umuhimu wa makampuni ya mafuta katita mji wa Sandnessjoen Meya wa mji huo Bard Anders Lango ameeleza kuwa mji wake unanufaika na mafuta na asilimia kubwa ya wananchi ni walipa kodi na asilimia 12 ya mapato urudishwa katika huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya.

Akiongea na globu hii,Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi Kelvin Makonda kwa Upande wake ametoa Shukrani kwa ujio huo na Kuanzishwa kwa ushirikiano baina ya miji hiyo na mikoa ya kusini kutasaidia kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na kuwezesha wananchi kuwa sehemu ya mafanikio ya kuanzishwa kwa miradi ya umma katika maeneo yao.

Huu ujio umekuja muda muafaka huku manispaa yangu kwa kushirikiana UTT tayari imepima Viwanja vya kutosha na tumeanza mchakato wa kuviuza na hata hawa wageni wetu tumewapa Fursa ya kununua viwanja kwa ajili ya shughuli za uwekezaji ikiwemo Hotel,Elimu na Viwanda maeneo yapo ya kutosha".

Katika ziara hiyo inayoongozwa na Balozi wa Norway nchini Tanzania,Bi Ingunn Klepsvik walitembelea Mabwawa ya Uvuvi ya ASM Trading 2005 na kumilikiwa na Abdillah Salum Mfaume ambayo tayari jumla ya Samaki 96468 wameshapandwa katika mabwawa hayo.

Aidha Bw Abdilah salum alitoa wito kwa ugeni Huo kusaidiwa utaalam wa kutosha katika Ufugaji wa Kutosha bila ya kuathiri Mazingira na kubainisha kuwa matarajio yake ni kuvuma zaidi ya kilo 25000 katika kipindi cha miezi sita ijayo hali itakayomwongezea kipato na kujiwezesha kuboresha Uvuvi katika mkoa wa Lindi

Wednesday, March 25, 2015

Wakulima washauriwa kuboresha zao la ALIZETI

Maduka makubwa mchanganyiko- SUPERMARKETS yamewashauri wakulima kuboresha kilimo cha zao la Alizeti kwa vile mafuta yanayotokana na zao hilo yana soko kubwa kuliko mafuta ya kutoka nje. 

Wakizungumzia ubora wa mafuta hayo, msemaji wa duka la Mirado Fortunatus Bernard na msemaji wa duka la TSN Nassoro Abdallah wamesema mafuta ya alizeti yanapendwa kwa sababu yanawasaidia watu wenye matatizo ya moyo.

KINANA aishauri serikali kufanya tathmini ya mashamba yaliyochukuliwa na wawekezaji

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi-CCM, ABDULRAHMAN KINANA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi-CCM, ABDULRAHMAN KINANA ameishauri serikali kufanya thamthni juu ya mashamba ya baadhi ya wananchi yaliyochukuliwa na wawekezaji ambao wameshindwa kuendeleza wakati wa kipindi cha ubinasfsishaji ili kuruhusu wigo mpana wa wananchi kupata fursa ya kumiliki ardhi. 

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa SANYAJUU, wilayani SIHA mkoani KILIMANJARO, KINANA amesema baadhi ya wawekezaji wakubwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo TANGA, ARUSHA na KILIMANJARO wamehodhi maeneo makubwa ya ardhi ambayo wamekuwa wakiyakodisha kwa wafanyabishara, mashamba ambayo hapo zamani yalikuwa yakimilikiwa na wananchi. 

Akiwa ziarani mkoa wa KILIMANJARO, katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ABDULRAHAMN KINANA, akatembelea katika bwawa la umwagilaiji katika kijiji cha KASHISHI wilayani SIHA, mradi ambao unatajwa kuwa chachu ya wananchi kujipatia kipato na kupitia sekta ya kilimo.
(imetolewa na tbc1)

MANYARA yakumbwa na ukame

Mkuu wa mkoa wa MANYARA, DOKTA JOEL BENDERA
Wakati hayo yakiendelea jijini DSM, huko Mkoani MANYARA hali ya ukame imekuwa tishio kwa wakulima Mkoani humo na kuwasababishia hofu ya kukabiliwa na njaa kutokana na uhaba wa mvua kwa kipindi kirefu. 

Baadhi ya wakulima wamesema uhaba huo wa mvua umesababisha mazao yaliyoko shambani hususan mahindi kunyauka. 

Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2014/2015, mkoa wa MANYARA umefanikiwa kuwa na mavuno ya uhakika ya mazao mbalimbali kutokana na mvua za wastani zilizonyesha kwa mpangilio 

Lakini katika msimu huu, kila mahali mkoani Manyara, wakulima wanapaza sauti zao za kukosa matumaini ya kuvuna chochote baada ya jitihada kubwa walizowekeza katika kilimo kuonekana kugonga mwamba. 

Wataalamu wa idara ya kilimo katika wilaya ya HANANG wameielezea hali hiyo ya ukame kutishia upatikanaji wa chakula 

Mkuu wa mkoa wa MANYARA, DOKTA JOEL BENDERA, amesema katika mahojiano maalumu na TBC, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia hali hiyo ya ukame 

Makundi mbalimbali ya kijamii yameanza kufanya ibada za aina mbalimbali zikiwemo za kimila na kwenye makanisa kuombea mvua inyeshe ili kunusuru hali hiyo

imetolewa na TBC 1


TANZANIA na KENYA zatiliana saini kudhibiti biashara haramu ya mazao ya misitu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Maliasili nchini Kenya Richard Lusiambe (wakwanza kulia) akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki nchini Tanzania Gladness Mkamba mara baada ya kutia saini makubaliano ya Tanzania na Kenya kupiga vita biashara haramu ya mbao pamoja na mazao ya misitu inayofanyika kupitia mipaka ya nchi hizo katika mkutano uliofanyika jijini Arusha na Kuandaliwa na Shirika la kimataifa la kulinda wanyama na viumbe hai World Wildlife Foundation (WWF) ambao n
Serikali za KENYA na TANZANIA zimetiliana saini makubaliano ya kudhibiti biashara haramu ya mazao ya mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na mbao na biashara ya mkaa 


Naibu Mkurugenzi wa Misitu nchini akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira GRADNESS MKAMBA,katika zoezi hilo jijini ARUSHA ambayo yamefadhiliwa na shirika la Uhifadhi wa masingira Duniani WWF,amesema makubalianao hayo yatasaidia biashara ya misitu inafanyika kwa kufuata sheria na si kwa njia za panya. 



Mara baada ya kusaini makubaliano hayo,Naibu Mkurugenzi wa Misitu ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira GRADNESS MKAMBA amesema biasahara haramu ya mbao na mkaa imekuwa ikifanyika kwa njia za panya na sasa kupitia makubaliano hayo itadhibitiwa. 



Katibu Mkuu anayeshughulikia mazingira na maliasili nchini KENYA, Dk RICHARD LESIYAMPE,amesema misitu inafaida nyingi kiuchumi na hivyo ni vema kuwe na utaratibu sahihi. 



Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Uhifadhi wa Mazingira Duniani WWF anayewakilisha nchi ya TANZANIA,AMANI NGUSALU,amesema nchi hizo zilikuwa na maeneo makubwa ya misitu lakini kwa sasa hali ni tofauti. 



Makubaliano kama hayo yalishafanyika baina ya nchi ya TANZANIA na MSUMBIJI mwaka 2013 na yanadaiwa na wataalamu wa misitu kuonyesha mafanikio makubwa.
(IMETOLEWA NA TBC1)

Monday, March 23, 2015

Welcome to Rifaro Africa ... Simu Yako, Jembe Lako

Welcome to Rifaro Africa ... Simu Yako, Jembe Lako

Who We Are

RIFARO AFRICA is a network marketing company that uses the direct selling method to distribute telecommunication products and services primarily and exclusively using an online platform. At Rifaro Africa, we not only sell products that people NEED but products that EVERYONE uses .In addition, it is evident that telecommunication companies spend billions to compensate the middlemen involved in airtime distribution, but when subscribers buy airtime on mobile money platforms none of the middlemen get the direct financial benefits. Rifaro Africa forms a club of members consuming products i.e. airtime, by buying through the Rifaro port on the mobile money platforms and passes the commissions back to members like you and me as incentives and commissions when you just sign up and promote Rifaro products as a Rifaro Africa Distributor.

Magadi chumvi yaathiri kilimo cha mpunga SAME

Magadi chumvi yaathiri kilimo cha mpunga SAME
Wakulima wa zao la mpunga wilayani SAME mkoani KILIMANJARO wamesema kilimo cha mpunga wilayani humo kimekuwa kikiathiriwa na uwepo wa magadi chumvi yanayoathiri rutuba katika mashamba yao na kupunguza uzalishaji wa zao hilo. 

Wakizungumza katika kikao cha wadau wa kilimo cha mpunga kilicho fanyika katika kijiji cha NDUNGU wilayani SAME wakulima hao wamesema magadi chumvi hayo yamekuwa ni changamoto kubwa jambo ambalo linaweza kupunguza kabisa uzalishaji wa mpunga katika kipindi cha miaka 20 ijayo. 

Daktari SOPHIA KILLENGA ambaye ni mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo ARI-KATRIN ameeleza athari za magadi chumvi katika kilimo cha mpunga pamoja na jia ambazo zinawezatumika kupunguza magadi chumvi katika udogo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa HALMASHAURI ya wilaya ya SAME CHRISTOPHER MICHAE ameeleza mikakati aliyoweka kutokana na kutambua uwepo wa tatizo hili. 

Zao la mpunga ni miongoni mwa mazao yanayolimwa kwa wingi hapa nchini ambapo utafiti unaonesha kuwa Tanzania ni ya pili kwa kilimo cha mpunga katika nchi zilizochini ya jangwa la sahara ikitanguliwa na nchi ya MADAGASCA.

Sunday, March 22, 2015

MILONGE (moringa oleifera)

Hii ni miti ambayo haiwi mikubwa sana, inakuwa na maua meupe na kisha hutoa mbegu ndogo zinazokuwa kwenye magamba marefu kama kisu. miti hii hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye mvua kiasi na joto, hustawi zaidi kwenye udongo usiotuamisha maji na inaweza kustawi kwenye udongo usio na rutuba nyingi na inahimili ukame kwa kiasi kikubwa.

SIDA yatoa msaada wa fedha kuendesha miradi ya kilimo


Shirika la Maendeleo la SWEDEN -SIDA limetoa EURO Milioni 2.5 kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki katika kuendeleza mradi wa uendelezaji biashara ya mazao ya kilimo hai. 


Mradi huo ambao utachukua takribani miaka minne 2015/2019 utazishirikisha nchi zote tano za Afrika Mashariki 

Akizungumzia mradi huo mjini Unguja,Mtendaji Mkuu wa Uendelezaji wa kilimo hai Tanzania JORDAN GAMA amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wakulima na wasindikaji wa kuzingatia ubora wa kuzalisha mazao ya kilimo hai.

Wajasiriliamali wa zao la mlonge kupewa elimu


Kampuni ya IDEAL HELATH CARE inayojihusisha na utengezaji wa dawa za mlonge inatarajia kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wakulima ya kuzalisha zao la mlonge kibiashara. 

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo JOHN KABUGI amesema katika mafunzo hayo wataweza kutoa elimu kwa wajasiriamali ya jinsi ya kulitumia zao hili ili kujiongezea kipato. 

KABUGI amesema kwamba pamoja na umuhimu wa zao hilo katika uzalishaji wa dawa za asili lakini bado halijaanza kulimwa kibiashara nchini.