Friday, November 23, 2012

MILONGE (moringa oleifera)

  Hii ni miti ambayo haiwi mikubwa sana, inakuwa na maua meupe na kisha hutoa mbegu ndogo zinazokuwa kwenye magamba marefu kama kisu. miti hii hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye mvua kiasi na joto, hustawi zaidi kwenye udongo usiotuamisha maji na inaweza kustawi kwenye udongo usio na rutuba nyingi na inahimili ukame kwa kiasi kikubwa.

MATUMIZI
Majani yake huweza kupikwa kama mboga na kuliwa, pia yanaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila ya kuathiri ubora wake wa virutubisho (nutritional value) majani yake yanavirutubisho vingi kuliko vyakula vingi tulivyozoea mfano


Ina vitamin A nyingi zaidi ya karoti
Ina Calcium nyingi zaidi ya Maziwa
Ina madini ya chuma zaidi ya spinach
Ina vitamin C nyingi zaidi ya Machungwa
Ina madini na pottasium zaidi ya Ndizi
ina protein nyingi zaidi ya nyama na mayai



MATUMIZI MENGINE
Maganda ya mbegu zake yanaweza kutumika kutibu maji(water treatment)unachukua maji yako ambayo unahisi si salama, unachanganya na maganda ya mbegu zilizopondwa pondwa kiasi, unayaacha kwa muda yatuame kisha unayachuja na yanakuwa salama kwa matumizi


Mbegu za milonge zinaweza kutumika kama dawa ya kupunguza sukari mwilini kwa wagonjwa wa kisukari, unachukua mbegu mbili au tatu unazipasua na kuchukua kokwa ya ndani na kutafuna mara 3 kwa siku, matumizi yanaweza kuongezeka au kuzidi kutegemeana na hali ya mgonjwa

Picha hapo chini inaonyesha mbegu za mlonge juu na kulia kwake ni baada ya kupasuliwa na kupata kokwa ya ndani (ambayo ni dawa ya kupunguza sukari mwilini), funguo imewekwa ili kujua ukubwa halisi wa mbegu


Sehemu yoyote ya mmea kama majani, magamba, mizizi, au maua yakipondwa pondwa na kupakwa kwenye sehemu yenye uvimbe ni dawa tosha ya kupunguza hali hiyo, pia dawa hii inauwezo mkubwa wa kupunguza sumu kama umeng'atwa na wadudu kama nyuki, manyigu/dondola, siafu, tandu, nge nk

Mbegu zake zinatoa mafuta (40%) yanayojulikana kama BEN OIL, ambayo hutumika kulainishia mitambo maalum kama saa za ukutani, pia mafuta haya ni dawa ya upele na harara

Wednesday, November 21, 2012

KILIMO CHA MATIKITI MAJI - watermelon

ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.

HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi machi mpaka septemba .

UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenye mifuko ya plastiki halafu ndo uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenyewe, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia

MCHE ULIOCHIPUA


UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi

MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi

UCHAVUSHAJI KWA MKONO


UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi


MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi

Tuesday, November 20, 2012

UGONJWA WA NAGANA - Trypanosiasis

Ugonjwa huu hushambulia karibia mifugo yote na pia binadamu, kwa binadamu ugonjwa huu hujulikana kama malale. ugonjwa huu husababishwa na vijidudu vya protozoa vijulikanavyo kama Trypanosoma evansi na kusambazwa na mbung'o au ndorobo (glossina spp) vijidudu hivi vikimuingia mnyama vinatumia kiasi kingi cha sukari kwenye mwili wa  mnyama na  kuharibu seli nyekundu za damu na kusababisha  upungufu mkubwa wa damu kwa mnyama.

DALILI

1-
Ugonjwa huu kwa ng'ombe unaweza kuwa wa hatari na  hata  kuwa sugu na kuleta madhara makubwa ikiwamo kifo
2
-Joto la mnyama hupanda hadi kufikia sentigredi 39 - 41
3
-Mnyama hupata tabu kuona huku akitoa machozi mengi kama anayelia
4
-Uzalishaji wa maziwa hupungua ghafla kwa kiasi kikubwa
5
-Mnyama hupumua kwa tabu kwa kutumia nguvu
6
-Mnyama huonyesha kuchanganyikiwa akili, anaweza kutembea kwa mduara, kupiga piga kichwa kwenye mabanda au chochote na mnyama  huweza kupoteza fahamu
7
-Baadhi ya wanyama wajawazito huweza kutoa mimba, hii ni kwenye ile hali ya ugonjwa sugu ambao hushambulia pole pole
8
-Kuvimba kwa matezi
9
-Manyoya ya ng'ombe mgongoni wakati wa asubuhi yana kuwa yanang'aa kwa aina fulani jua likiwaka, ila inahitaji uonyeshwe na wataalam kwanza

NG'OMBE AINA YA N'DAMA



UCHUNGUZI

Maafisa ugani wa mifugo watachukua sampuli za damu kutoka kwenye mkia au sikio la mnyama na vijidudu kuonekana kwa darubini ya umeme mkali kabla ya damu kukauka, pia njia ya kimaabara ya GIEMSA itasaidia
kwa uchunguzi zaidi wa kimaabara wadudu wanaweza kupandikizwa kwenye sungura, panya na simbilisi/pimbi na baadae njia ya PCR, ELISA kutumika kuangalia vichochezi vya mwili

TIBA

Kwa mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, jamii ya farasi, mbwa na paka dawa kama diminaphen, diminakel hutumika kutibu ugonjwa huu, kwa upande wa binadamu sifahamu dawa gani inatumika


KINGA

1
- Kuna njia ya kitaalam ijulikanayo kama sterile male technique, ambapo madume ya mbung'o hupigwa na mionzi ya gama na kushindwa kuzalisha yanapo panda, hii husaidia sana kwa sababu majike ya mbung'o hupandwa mara moja tu katika maisha yao wakati madume haya tasa huendelea kupanda majike tofauti tofauti
2-
Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu zinaweza kukinga wanyama kama watapigwa kila baada ya miezi mitatu na mara 4 kwa mwaka
3-
Kuna jamii ya ng'ombe wanaojulikana kama N'DAMA ambao hupatikana Afrika ya magharibi, aina hii ya ng'ombe inastahimili sana ugonjwa huu