Wednesday, January 29, 2014



VIDEO YA MTENDAJI MKUU WA SAGCOT AZUNGUMZIA HALI YA UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI


BONYEZA HAPA KUONA


Kenya yapiga jeki kilimo



 Kenya imezindua mradi mwengine tena ambao ikiwa utafanikiwa utapiga jeki na kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo nchini humo.

Mradi huo 'Galana Kulalu' katika mkoa wa pwani unanuiwa kuziweka katika mpango wa unyunyiziaji maji ekari zaidi ya millioni moja za kilimo hasa cha mahindi na miwa.
Mradi huu unakadiriwa kwamba katika kipindi cha miaka 5 ijayo utagharimu zaidi ya shilingi billioni 250 za Kenya.
Tangu kale maeneo ya bara ya Kenya ndio yamejulikana kuwa na kilimo kinacholisha nchi kutokana na hali nzuri ya hewa na kupata mvua ya kutosha , lakini mpango huu wa Galana Kalula unasemekana utaifanya Kenya kuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula na hata kuweka kukiuza nje.
Kila ekari kwa mfano itatarajiwa kuzalisha kati ya magunia 40 na hamsini kutokana na rutuba ya ardhi hiyo na kunyunyiziwa maji kwa kipimo kinachohitajika.
Eneo hilo liko katika majimbo ya Kilifi na Tana river ambayo kwa miaka mingi yamekumbwa na umaskini na yameachwa nyuma kimaendeleo licha ya kuwa na ardhi nzuri ya kilimo.
Hii ilitokana na sera mbovu, ukosefu wa usalama na hivi majuzi kukumbwa na vita kati ya wakulima na wafugaji vilivyochochewa zaidi kisiasa.
Hadi sasa bado kuna hofu miongoni mwa wenyeji kwamba licha ya kuahidi mengi mazuri , huenda wasitendewe haki. Hata hivyo wadadisi wanasema iwapo mradi huo , utatekelezwa kwa haki na uwazi ni fursa nzuri ya kutatua matatizo yanayoilemea kaunti hiyo.

Tuesday, January 28, 2014


 RAIS KIKWETE AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NMB KATIKA MPANGO
WA KILIMO STAKABADHI GHALANI



Rais kikwete akisalimiana na mkuu wa kitengo cha masuala ya kilimo katika benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipo tembelea banda lao baada ya kufungua kongamano la kilimo Africa mashariki katika Hoteli ya kilimanjaro.




Rais Kikwete akipata maelekezo juu ya mpango wa stakabadhi ghalani ulivyo na manufaa kwa mkulima toka kwa mkuu wa kitengo cha masuala ya kilimo bw. Robert Pascal