Saturday, March 14, 2015

 Mmoja wa Wakulima wa Ufuta katika Kijiji cha Misima wilayani Handeni Bw. Rashidi Dempombe, akimweleza afisa Kilimo wa wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, kwa namna alivyolima na kupanda zao hilo ambalo ni la biashara.


 Mmoja wa wakulima wa nanasi wilayani Handeni Bi Sabrina Rory Sasumua, akionyesha aina ya nanasi lenye uzito wa kilo mbini na nusu kutoka katika shambani lake eneo la Kwamsisi wilayani Handeni.

MASHAMBA YALIKO HANDENI

 Sehemu ya mashamba ya mahindi katika maeneo mbalimbali wilayani Handeni.

Friday, March 13, 2015

UGONJWA WA MATUPA KWENYE MAHINDI (SMUT).




    Ugonjwa huu hushambulia sehemu za uzazi za mahindi. Mashambulizi hufanywa na aina mbili za vimelea jamii ya uyoga (ukungu) vijulikanavyo kwa majina ya kitaalamu kama Sphacelotheca reliana  na Ustilago maydis. Vimelea hivyo husababisha magonjwa ya aina mbili ambayo dalili zake zinafanana.
    Mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa huu ama haizai kabisa ama inazaa kiasi kidogo ukilinganisha na jinsi ambavyo ingeweza kuzaa kama isingekuwa imeshambuliwa. Kwa hiyo mashambulizi ya magonjwa haya husababisha hasara ya mavuno. Inakadiriwa kwamba hasara ya mavuno inawezakuwa kidogo tu ama asilimia kumi (10%) au hata zaidi ya kiwango hicho, lakini kupoteza ni kpoteza hata kama ni kiwango kidogo.
    Ugonjwa wa "matupa" unaosababishwa na kimelea kijulikanacho kama Ustilago maydis hufahamika kama "Common Smut" kwa kiingereza. Dalili zake huwa kuota kwa uvimbe katika sehemu za mmea zinazokua kama vile punje za mahindi, mbelewele na hata kwenye majani. Uvimbe huo ukikauka na kupasuka hutoa vumbi jeusi kama masizi ambayo ndiyo viini vya/mbegu ya huo ugonjwa. Dalili ya msingi ya ugonjwa huu kwenye mhindi ni kwamba inawezekana kuwa na baadhi ya punje zilizoshambuliwa na zingine ambazo hazina dalili katika gunzi moja. 
   Ugonjwa wa "smut" unaosababishwa na kimelea kijulikanacho kwa jina Sphacelotheca relianahufahamika kama "Head smut" kwa kiingereza. Kama ilivyo kwa ugonjwa wa "smut" ya kawaida, dalili za ugonjwa huu hujitokeza mara nyingi katika hindi lenyewe  na mbelewele na mara chache katika shina la mhindi. Tofauti na ugonjwa wa "smut" ya kawida, katika ugonjwa huu badala ya mhindi kuathiriwa baadhi ya punje, hindi zima hujaa vumbi jeusi ndani ambapo kwa nje ni kama mfuko mweupe ambao kabla ya kukauka hufana na uyoga. Vumbi hilo jeusi ndilo viini vya kimelea. Vivyo hivyo kwenye mbelewele. Wakati mwingine mmea ulioshambuliwa na ugonjwa huu hudumaa na hushindwa kuzaa. Dalili nyingine ya ugonjwa huu ni mhindi kuotesha vijani vidogo badala ya mbelewele.
                                            

    Dalili za ugonjwa wa "Head smut"
    UDHIBITI WA MAGONJWA YA"SMUT" 
1. Tumia mbegu bora ingawa mpaka sasa haipo mbegu maalumu yenye kustahimili ugonjwa huu. Kwa kutumia mbegu bora, mkulima utajihakikishia  mavuno bora.
2.  Daima hakikisha unalima kilimo cha kisasa kikijumuisha urutubishaji wa udongo. Epuka kuijeruhi mimea uwapo shambani. Mimea iliyo na majeraha hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa huu. Pia dhibiti wadudu waharibifu ambao pamoja na madhara  mengine wanayosababisha pia huijeruhi mimea na kwa hivyo kurahisisha maambukizo ya ugonjwa huu wa "smut".
3.  Kila inapowezekana tumia kilimo cha kubadilisha mazao. Katika kubadilisha mazao ni vema kutumia mzunguko wa mazao yasiyoshambuliwa na ugonjwa wa "smut" kama vile ngano, shayiri, njegere, viazi na maharagwe.
4.  Unapolima hakikisha masalia mabua yamefukiwa chini sana.
Nawatakia wakulima wote maandalizi mema ya msimu wa kilimo.

Mgogoro baina ya mwekezaji na Jamii ya wafugaji wapata ufumbuzi

Mkuu wa wilaya ya BABATI mkoani MANYARA, KHALID MANDIA, ametegua kitendawili cha muda mrefu juu ya mgogoro baina ya mwekezaji wa Kifaransa na Jamii ya wafugaji wa kabila la KIBARBAIG, katika kijiji cha VILIMA VITATU wilayani humo na kuwaruhusu waendelee na shughuli zao za ufugaji kwenye eneo ambalo mwekezaji huyo amelihodhi kinyume cha sheria. 
MANDIA ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na mwekezaji huyo anayemiliki hoteli ya kitalii ya UN LODGE, pamoja na wafugaji walioweka kambi porini kwa zaidi ya siku nne wakitaka kupatiwa majibu na serikali kuhusu utata wa umiliki wa eneo la mwekezaji huyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya BABATI, DOMINIC KWEKA amefafanua kuwa Halmashauri ya wilaya yake imepima eneo halali la ekari 45 la mwekezaji huyo na kuweka alama ili kuondoa utata huo. 
Mkuu wa wilaya ya BABATI, KHALID MANDIA akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, amewataka wafugaji hao kusimamia amani na utulivu katika eneo hilo na kuzionya pande hizo mbili kuacha kujichukulia sheria mkononi. 
Baada ya kumalizika kwa mkutano wa ndani kati ya kamati ya ulinzi na usalama na mwekezaji huyo kuhusu suala hilo, msemaji wa kampuni hiyo ya UN LODGE, LEONARD WEREMA amekataa kuzungumzia yaliyojiri katika mkutano huo.

Thursday, March 12, 2015

Wakazi wa MTUMBA wauza mashamba yao kwa wachimba mchanga


Wakazi wa vijiji vya MTUMBA na IHUMWA vilivyopo katika Manispaa ya DODOMA wameamua kugeuza mashamba yao kuwa vitega uchumi kwa kuwauzia wafanyabiashara wa kuchimba mchanga. 

Mbali ya shughuli hiyo ya kuchimba mchanga kuathiri mazao yakiwemo yale ya chakula, pia inatishia uharibifu wa mazingira. 

Mkoa wa Dodoma unaopata mvua chache za msimu, ambazo kwa kiasi kikubwa huathiri pato la mkulima kutokana na kutokuwa na mavuno ya kutosha. 

Baadhi ya wafanyabiashara wa mchanga wamekiri kuchimba mchanga kwenye mashamba ya watu wakidai kupata vibali na leseni kutoka wizara ya Nishati na Madini pia wanadai kuwepo kwa mkanganyiko baina ya manispaa na wizara ya nishati na madini kuhusu vibali. 

Pamoja na katazo la kuchimba mchanga kwenye mashambani ,bado manispaa imeendelea kutoza shilingi elfu kumi kama ushuru wa mapato kwa kila lori la mchanga,hata hivyo wanakiri kuwepo kwa athari.

Airtel yatoa msaada kwa wahanga wa mafuriko Kahama

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu 35 walifariki na kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu

Akionge wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na wanafamilia kutokana na mafuriko haya.

Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza . Leo kwa niaba ya Ofisi yetu ya kanda ya Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro pamoja na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

Sambamba na mchango huu, tunapenda kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa hii kuwaomba wateja wetu kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda namba 15626 , ujumbe huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga,

Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kahama helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati tunauhitaji zaidi, Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa watanzania kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.

Wednesday, March 11, 2015

Mfumuko wa bei ya chakula wapungua.

Na Josephine Mwaiswaga,
Dar es salaam. 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza kushuka kwa kasi ya Mfumuko wa Bei iliyojitokeza kwenye Bidhaa mbalimbali katika mwezi Desemba mwaka jana ambao ulikuwa asilimia 4.8 hadi kufikia asilimia 4.0 kwa Mwezi Januari mwaka huu. 
Mkurugenzi wa takwimu za idadi za watu na huduma za kijamii Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumko wa bei hizo kumetokana na kushuka kwa kasi kwa bei za bidhaa za vyakula, Unga, mafuta ya taa Deseli na Petroli. 
Akianisha mwenendo wa kupungua kwa bidhaa mbalimbali katika kipindi cha Mwezi Januari Mwaka huu, Kwesigabo amesema bei za mahindi zimepungua kwa asilimia 13.3, unga wa mahindi asilimia 6.2 , Samaki asilimia 7.9 ndizi za kupika asilimia 11.3 na mihogo asilimia 12.0. 
Aidha ofisi hiyo ya takwimu imeanishwa kuwa mafuta ya taa yameshuka kwa asilimia 8.4,dizel asilimia 10.2, Petrol asilimia 6.8 wakati gasi ya kupikia imeshuka kwa asilimia 2.1 
Aidha, Ofisi hiyo ya pia ikaanisha hali ya mwenendo wa bei katika Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania. 
Mbali na kupungua kwa kasi ya mfumko wa bei katika bidhaa zilianishwa, ofisi hiyo imeainisha kuwa bidhaa za mchele, nyama, lishe ya watoto na mbogambogo bado zimeonekana kuwa juu

SASA NI ZAMU YA WAKULIMA NA NMB

Benki ya NMB ndio benki pekee yenye matawi katika kila wilaya hapa nchini.Hivyo basi ndio benki pekee inayowajali wateja wake kwa kua karibu zaidi wakati wote.NMB imekua ikiandaa semina elekezi kwa wateja wake .Sasa ilikua zamu ya wakulima na wadau wote wa kilimo cha kahawa wameweza kupata fursa ya kujua huduma mbali mbali zitolewazo na NMB 
kwa ajili ya wakulima na wadau wote wa hudiuma za kibenki.Hivi karibuni NMB iliandaa semina kwa ajili ya wadau wa biashara za Kilimo ambayo 
imeendeshwa katika mikoa mbali mbali ikiwmo Tabora na Mbeya

Watu wasiojulikana wachoma shamba la muwekezaji mkoani MANYARA


WATU wasiofahamika wamechoma moto na kuteketeza mali za mwekezaji wa Shamba la HAMIRE ESTATE, lililoko katika eneo la Bonde la KIRUSIX wilayani BABATI mkoani MANYARA, usiku wa kuamkia tarehe 09 March, 2015 
Mali zilizoteketea ni pamoja na Matrekta matatu na nyumba moja iliyokuwa ikitumiwa kama ofisi katika eneo la Mwekezaji huyo 
Tukio hilo litawaweka kando na kazi au kibarua zaidi ya wafanyakazi 200 
waliokuwa wakitegemea kipato chao kila mwezi kwa kufanya kazi katika shamba hilo 
Baadhi ya wenyeji wa eneo hilo akiwemo diwani wa kata ya KIRU, FABIANO TLANKA, wamelaani matukio hayo ya uchomaji moto mali za wawekezaji 
Mbunge wa BABATI VIJIJINI, JITU SONI, ameitaka serikali kudhibiti vitendo hivyo vinavyotishia usalama wa wawekezaji walioko katika Bonde hilo 
Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Mkoani MANYARA, JUSTINE MASEJO, amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linachunguza kuhusu tukio hilo 

Wakulima wanufaika na mbegu za kisasa za Viazi


Wakulima zaidi ya 2,700 wa mikoa ya NJOMBE, IRINGA na MBEYA, wameanza kunufaika na Mradi wa Uzalishaji wa mbegu za kisasa za viazi Mviringo, Mradi ambao unatekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole kwa kushirikiana na na serikali ya Finland. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Dkt. ZAKARIA MALLE, amesema mradi huo wa miaka Mitatu tayari umefanya utafiti na kugundua mbegu Nne za aina za Viazi Mviringo ambazo zinastahimili magonjwa ukilinganisha na mbeguu zilizoletwa na wakoloni ambazo hazina tija kwa wakulima. 
Zao la Viazi Mviringo linastawi kwa wingi katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa, tayari wakulima zaidi ya 2,700 wa wilaya za Kilolo, Mufindi, Waking’ombe,Njombe na ,Mbeya wamenufaika na mradi wa uzalishaji wa Mbegu bora za kisasa za viazi mviringo. 
Uboreshaji wa kilimo cha viazi mviringo, ni mpango wa wizara ya kilimo chakula na ushirika kumwezesha mkulima kuwa na uzalishaji wenye tija kuuza viazi ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Tuesday, March 10, 2015

Wakulima mkoani DODOMA waiomba serikali miradi ya umwagiliaji

Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi, ABDULRAHAMN KINANA
Kufuatia Mkoa wa DODOMA kukabiliwa na ukame katika maeneo mmbalimbali, baadhi ya wananchi wilayani CHAMWINO mkoani humo, wameiomba Serikali kuwasadia wakulima miradi ya umwagiliaji, hali ambayo itaongeza tija ya mazao mbalimbali yatokanayo na kilimo ndani na nje ya wilaya ya hiyo.

Wakizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi kutembelea wilayani humo, wananchi hao wamsema wakulima wengi wa zabibu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto hiyo na kusababisha uzalishaji za zabibu kutokuwa na tija kama ilivyokusudiwa.

ziara ya Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi, ABDULRAHAMN KINANA hapo jana alitembelea katika shamba la zabibu linalomilikiwa na ushirika wa kikundi cha baadhi ya wananchi wa wilaya ya CHAMWINO.

Kisha KINANA akashiriki kupuliza dawa ya kuua wadudu wanaoshambulia zabibu akionyesha kuunga mkono jitihada za kilimo hicho.

Kwa upande wake KINANA, hakusita kutilia mkazo suala la kilimo cha umwagiliaji na uhifadhi wa mazingira kwa wakulima hao

KABICHI NI KINGA DHIDI YA SARATANI

Ugonjwa wa saratani (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo.

Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maalum kwa ugonjwa huu.

Katika makala ya leo, tutajifunza faida za kabichi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, licha ya kuchukuliwa kama ni mboga ya kimaskini na ambayo huliwa kwa shida zaidi kuliko kimanufaa ya kiafya.

Ingawa inaonekana kuwa kabichi ni miongoni mwa mboga za majani zinazolimwa kwa wingi na kusambazwa kwenye masoko mengi nchini, hasa katika miji mikubwa, lakini ni watu wachache sana wanaopenda kula mboga hii.

Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumia ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.

 KINGA DHIDI YA SARATANI
Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani.

Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.

Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho;
‘Antioxidant’, ‘Anti-inflammatory’ na ‘Glucosinolates,’ ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.

AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO
Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.

HUIMARISHA MFUMO WA MOYO
Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.

VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHI
Ndani ya kabichi, kuna kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Ili kupata faida za kabichi na kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.

Wafugaji watakiwa kuacha kuweka alama za moto kwenye ngozi

Naibu waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi KAIKA SANING’O TELELE
Naibu waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi KAIKA SANING’O TELELE amezungumzia umuhimu wa wafugaji nchini kuacha tabia ya kuweka alama ya moto kwenye ngozi za mifugo yao ili kulinda ubora wa ngozi za mifugo hiyo. 
Akizindua kamati ya kitaifa ya ushauri wa ngozi jijini DSM , Telele amesema ngozi nyingi zinazozalishwa nchini hazina ubora unaotakiwa kwa sababu zimewekwa alama za moto. 
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamewashauri wafugaji kuzingatia kanuni za ufugaji bora wa mifugo ili kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yatokanayo na mifugo yao. 

Monday, March 9, 2015

MH PINDA ATEMBELEA SOKO LA MIEMBENI MJINI DODOMA


Waziri Mkuu Mizengo pinda akikagua bei ya mahindi katika soko la Miembeni mini Dodoma mach 8,2015 alipita sokoni hapo kukagua upatikanaji wa vyakula
Waziri mkuu mizengo pinda akiwapa maelekezo kuhusu kilimo cha zabibu walimu wa shule za kata ya zuzu dodoma waliokwenda shambani kwake mach 8,2015 ka ziara ya kujifunza (picha na ofisi ya waziri mkuu

UFUGAJI WA KUKU: UMUHIMU WA KUWA NA VIOTA BORA

Kuku anapotagia porini, mayai huliwa na wanyama kama vile nyoka na wengineo. Kuku pia anaweza kudhuriwa na wanyama hao na wakati mwingine kuibwa.

Viota ni mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuhatamia na kuangua vifaranga. Hii inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga. 
Aina za viota
Kuna makundi mawili ya viota vinavyotumiwa na kuku pamoja na ndege wengine wafugwao.
• Kiota kilicho tengenezwa na kuku mwenyewe

Hii ni aina ya viota ambavyo kuku huchagua mahali pa kutaga na kuhifadhi mayai. Inaweza kuwa mahali popote ambapo kuku ataona mayai hayataweza kudhurika au kuonekana. Kwa mfano, vichakani, stoo au kona yenye giza. Njia hii si nzuri kwani husababisha upotevu wa kuku na uharibifu wa mayai.
Kwa kutagia stoo au sehemu iliyojificha ya ndani, japokua ni sehemu salama ambayo haiwezi kufikiwa kirahisi na wezi au wanyama, mayai yanaweza kuharibika. Kuku akitaga sakafuni, sehemu yenye nailoni au magunia mayai yanaweza kuharibiwa na unyevu. Mayai hayo si mazuri kwa kutotoleshea. Itabidi mfugaji ayatumie au ayauze kwa ajili ya chakula.
Katika ufugaji wa ndani, kuku hutaga mayai sehemu yoyote hasa kipindi ambacho kuku huanza kutaga. Hii husababisha mfugaji kuyakanyaga mayai kwa bahati mbaya au kuku wenyewe kula mayai hayo na kupunguza uzalishaji wa mayai.
• Kiota kilicho andaliwa na mfugaji
Kuku wanapotengenezewe viota vizuri huhatamia kwa utulivu kuongeza uzalishajiHii ni aina ya viota vilivyo andaliwa kiustadi na kuwekwa mahali stahiki kwa kumrahisishia kuku sehemu ya kutagia. Viota hivi huwekwa ndani ya banda au sehemu nyingine iliyoandaliwa. Viota vya aina hii huandaliwa kwa kuzingatia idadi ya kuku wanaotarajiwa kutaga, pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kutengeneza viota.
Mahitaji
Unaweza kutumia vifaa kama vile boksi la karatasi, mbao, nyasi, nguo aina ya pamba (isiwe ya tetroni), matofari na maranda. Boksi, tofali, na mbao husaidia kutengeneza umbo na ukubwa wa kiota. Nyasi maranda na nguo (viwe vikavu) husaidia katika uhifadhi wa mayai yasiharibiwe na unyevu, pia ni mazuri kipindi cha kuhatamia kwani hutunza joto.
Ukubwa wa kiota unatakiwa uwe ni wa kumwezesha kuku kuenea na kujigeuza. Hii ina maana kuwa unatakiwa uwe wastani wa sentimita 35 upana sentimita 35 na urefu sentimita 35.
Namna ya kupanga viota kwenye banda
Ili kuwa na ufanisi mzuri, inabidi idadi ya viota kwenye banda iwe robo tatu ya matetea yaliyofikia umri wa kutaga. Hii huondoa msongamano wa kutaga katika kiota kimoja. Kwa mfugaji mwenye kuku wengi inampasa kuchagua vifaa ambavyo atajengea viota vinavyoweza kutumia eneo dogo na huku akipata viota vingi.
Kwa kuku wanaohatamia, inabidi watengewe chumba chao ili kuzuia uchanganyaji wa mayai. Kila sehemu katika banda si nzuri kuweka viota. Hivyo, katika uchaguzi inakupasa uzingatie mambo yafuatayo:• Viota visiwe karibu au chini ya kichanja cha kupumzikia, vyombo vya chakula na maji.• Kiota kisiwe sehemu ambayo mfugaji atakua anapitapita. Mfano, karibu na mlango au dirisha.• Kiota kisiwe mkabala na sehemu ambayo upepo mkali au mwanga utakua unaingia.
Wakati wa ujenzi wa banda unaweza kujenga vyumba viwili ambavyo kimoja kikubwa utatenga sehemu ya chakula, maji na sehemu ya kupumnzika. 

 
Chumba cha pili utatengeneza viota tu ili kuku anayetaka kutaga aende huko. Kwa kufanya hivyo, kuku wachache watakua wakienda chumba hicho, na usumbufu kwa kuku wanaotaga utakuwa mdogo.Kulingana na kiasi cha nafasi, unaweza kujenga viota mwisho wa banda na vyombo vya chakula na maji upande wa mbele karibu na mlango. Hii itasaidia kuku kushinda sehemu yenye chakula na maji hivyo kuepusha usumbufu kwenye viota.
Kuku wanaohatamia
Viota vya kuku wanaohatamia inabidi viwe sehemu tofauti na viota ambavyo kuku wanatagia mayai kila siku. Hii itasaidia kuzuia uchanganyaji wa mayai yaliyoanza kuhatamiwa na mapya. Viota hivyo viandaliwe vizuri kwani hukaa na mayai kwa muda mrefu. Ni vema kuwatenga kuku katika chumba chao ambapo watapatiwa maji na chakula.
Umuhimu wa viota
• Kwa kuwa na viota vya kutosha itapunguza usumbufu wa kuingia kukusanya mayai kwa mfugaji.• Njia mojawapo ya kuzuia kuku kula mayai.• Upotevu wa kuku na mayai utapungua.• Utapata mayai bora kwa ajili ya kutotolesha.• Kupunguza mayai kupasuka, pia mayai kuwa safi.
• Kuku kuwa huru wakati wa kutaga au kuhatamia.

Sunday, March 8, 2015

UFUGAJI WA KISASA VIJIJINI UNAWEZEKANA


IMG_0754
Kuna wafugaji wengi tu wenye imani/dhana kwamba ufugaji wa kisasa vijini hauwezekani kulingana na utunzaji wake. Mfano huu wa Bwana Aidan Paulus wa huko Mbinga utatupa fundisho zuri tu wafugaji wenye imani ya aina hii. Kikubwa ni kuweka jitihada na moyo wa kuthubutu. Yeye amethubutu na ameweza, wewe je?
Ni ndani ya shamba ambalo kiukweli ni msitu wa ukweli ambao ni takribani kilomita za mraba 50 na humo anaishi mwenye shamba Bw. Aidan Paulus Kenyero katika kijiji cha Liganga, wilaya ya Mbinga.
Bwana huyu pamoja na kujihusisha na kilimo cha mazao lakini pia anafuga mifugo…ngómbe zaidi ya 70 na vitu vingine. Nimejifunza namna ya kuhudumia kuku wa mayai na kuepusha mayai kuvunjika pindi yakishatagwa.
Bwana huyu ana nyumba ya ghorofa moja ilojengwa humo msituni mwaka 1989 na anatumia umeme wa gesi (Biogas) ambapo ana mitambo 2. Anacho pia kiwanda cha sukari lakini hakifanyi kazi kutokana na ukiritimba wa serikali hivo amekifunga na mitambo ipo tu imelala
IMG_0755
Kuku wa mayai…anao pia kuku wa kienyeji
IMG_0757
Baadaye kwenye ‘drowa’/saraka ya chini mayai hayo hufichwa
IMG_0758
Kuku akipanda juu akienda kushusha mzigo

UGONJWA WA MIDOMO NA MIGUU (FOOT AND MOUTH DISEASE)


Cow infected with FMD
Huu ni ugonjwa unaowashika ng’ombe, kondoo, mbuzi, pamoja na wanyama wa porini kama mbogo, swala na wakati mwingine tembo.

Ng’ombe anapopatwa na ugonjwa wa miguu na midomo huchechemea na asipotibiwa kwa haraka hushindwa kusimama na kula hatimae hudhoofika na hata kufa.
Ugonjwa wa miguu na midomo husambaa haraka kwenye kundi ukiua ndama na kusababisha wanyama kupoteza uzito na uzalishaji wa wengine kupungua.
Namna unavyoambukizwa
Ugonjwa huu unaambukiza kwa kugusana kwa mnyama mmoja na mwingine. Unaweza vile vile kusambazwa na upepo kwenye umbali hata wa kilometa 250. Pamoja na kusambaa kwa umbali huo, ni nadra kwa binadamu kupata ugonjwa huu.
Kwa muongo mmoja uliopita, wastani ugonjwa huu ulikuwa unashambulia kundi mara moja kwa mwaka. Kwa sasa, katika sehemu nyingi za Afrika Mashariki, ugonjwa unatokea mara tatu kwa mwaka. Aidha, jinsi hali ya hewa inavyokuwa ya joto la juu, yanatokea matabaka mapya ya vimelea visababishavyo ugonjwa huu.

Dalili
• Kuwepo mifugo yenye dalili za mafua, na kuchechemea kwa wakati huo huo.
• Ndama kufa kwa ghafla kutokana na ugonjwa wa moyo.
cow-infected-with-fmd
Tahadhari
Ugonjwa wa miguu na midomo una madhara makubwa kiuchumi hasa ukizingatia kuwa, uzalishaji wa maziwa wa ng’ombe waweza kupungua kwa asilimia 75 kwa maisha yake yote.
Mbali na hayo, ng’ombe badala ya kuzaa kila mwaka au kwa vipindi kama hivyo, anaweza kuzaa kila baada ya miaka miwili au mitatu.

Namna ya kuzuia
Chanjo kwa ajili ya ugonjwa huu husaidia kuzuia isipokuwa gharama yake ni kubwa kwani chanjo hizo zinanunuliwa kutoka nchi za nje na lazima iwe ya kufanyakazi dhidi ya aina nyingi za vimelea. Hata hivyo, jamii inaweza kupanga, na kununua chanjo kwa kushirikiana.
Ugonjwa wa miguu na midomo ni tishio, hasa katika maeneo ambapo mifugo inatumia ardhi ambayo pia inatumiwa na mbogo na nyumbu. Ni vyema kwa wale wanaoishi katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa ardhi wanayotumia kulishia mifugo yao si ile inayotumiwa na wanyama pori

SHUBIRI MWITU (ALOE) TIBA YA MAGONJWA YA KUKU

Shubiri mwitu (Aloe) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa kutmia mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonyesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani.
Picha ya mmea wa Shubiri mwitu. Mmea huu unaweza kupandwa nyumbani kama ua kwenye ndoo au kupandwa ardhini kama mimea mingine.
Maji maji ya mmea huu yanauwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.Mmea wa aloe vera unaweza kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake na unakubali maeneo karibu yote.Majina ya mmea huu kulingana na baadhi ya makabila na kimataifa

Jina la Mmea
Lugha
Shubiri mwitu
Kiswahili
Mkankiruri
Kinyaturu
Itembwe
Kigogo
Ibhata
Kinyiha
Litembwetembwe
Kihehe
Koli
Kikaguru/Kinguu
Aloe
Kiingereza
Aloe vera
Kisayansi

Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kukuKulingana na tafiti zilizofanywa na Bejar (Chuo kikuu cha Kilimo na Misitu cha Samar) na Clapo (Chuo Kikuu cha Ufilipino Mashariki) inaonyesha kuwa ziada ya Shubiri mwitu kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka. Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yanauwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na kuongeza uzito wa ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.Uandaaji wa Shubiri mwitu Kunjwa: Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3 kutegemeana na idadi ya kuku. Viache humo kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama unakuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.
Vidonda:Kuku wenye vidonda kama kwa ugonjwa wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na kuvichekecha ili upate unga laini. Uanike na kisha tunza vizuri tayari kwa kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye vidonda hivyo.

UTI WA MGONGO WA TAIFA UMEKUFA

 Habari ndugu zangu watanzania, ni matumaini hamjambo nyote. Poleni na shughuli za ujenzi wa Taifa, wakulima wanahangaika kuandaa mashamba maana maeneo mengi ya nchi mvua zimeanza kunyesha sasa, poleni sana na nawaomba muongeze nguvu zenu mashambani. Ndugu zangu, leo hebu tujaribu kuangalia hili la kwamba walau kila mtanzania ama anajua, amesikia au kuambiwakuwa Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa. Wakubwa, wenye mamlaka wamekuwa wakituimbia kila leo huo wimbo, ni wimbo mzuri sana, lakini je wanaouimba na kuutangaza unatoka mioyoni mwao na kweli uko akilini mwao hasa? Hebu kila mmoja wetu ajiulize mara mbili mbili wakati tunaenda kulijadili hili.

  Kwanza kabisa nakubaliana na hoja hiyo ya kwamba Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu (Tanzania). Na naelewa na kuamini kwamba mlinzi hasa wa uhai wa uti wa mgongo huu si mwingine bali Mkulima, tena si mkulima tu, Mkulima mdogo mdogo wa huku vijijini. Ndugu zangu ili tuite Kilimoni uti wa mgongo kuna vitu na mambo mengi ya kufanya kwenye hilo na si kusema tu kwa maneno.
  Mkulima anakabiliwa na changamoto nyingi sana kwenye Kilimo chake. Ili mkulima apate tija katika kilimo chake kuna vitu vinavyohitajika shambani, yaani mbolea, mbegu na madawa (Pembejeo). mkulimanamfugaji1@gmail.comPembejeo zinahitaji pesa. Mkulima anahangaika huku na kule kudunduliza kupata mbolea, changamoto nyingi anazipata wakati akihangaika kupata pembejeo ni pamoja na kupata pembejeo feki ama zimechakachuliwa au zimekwisha muda wa kutumika. Huyu mkulima anapovuna mazao yake, je soko la uhakika la mkulima huyu liko wapi? ni dhahiri shairi halipo, anahangaika tena kutafuta soko, sokoni ananyanyaswa, anapangiwa bei ya mazao yake na wafanyabiashara, hana haki tena katika mazao yake. Mfanyabiashara huyu anayempangia mkulima bei ya mazao yake, amemsaidia nini katika kuzalisha mazao yake? hakipo alichomsadia. Kwa nini basi serikali isidhibiti, kuratibu na kusimamia utaratibu wote wa masoko ili kulinda maslahi ya mkulima na mazao yake.
  Katika hilo la wajibu wa serikali, ni mipango mingi ya kumhusu mkulima anayoibuliwa, lakini utekelezaji wake ni hafifu kiasi flani. Ni kweli kwamba kuna tatizo la rasilimali Pesa katika nchi yetu maskini yenye rasilimali kibao, lakini kama kweli tunaimba huu wimbo wa kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa ni lazima tuhakikishe kwamba pesa inayohitajika kwenye kilimo itoke katika pesa ya ndani, na syo kutoka kwa wahisani ambao wanatoa masharti ya jinsi ya kuzitumia kwa matakwa yao na ya nchi zao. Katika hili lazima wenye mamlaka wajue kwamba Tusikubali watu wetu washibishwe na Wazungu. Hebu sasa tujiulize kama watanzania, tuko wapi katika kilimo na tunataka kufika wapi?
  Suluhisho la jambo hili ni kuhakikisha kwamba mkulima analima kwa tija na anapata soko la uhakika kwa kuwekewa mazingira shirikishi katika kilimo chake. Hayo ni maoni yangu, toa maoni yako mkulimanamfugaji1@gmail.comukimlenga mkulima na kilimo chake ukilinganisha na wimbo huu  "kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa"

FAIDA YA MBOGA MBOGA KWA AFYA


Mboga ni moja ya vyakula vilivyo muhimu sana kwa uhai wa afya ya binadamu. Mara nyingi mboga hutumiwa kama kitoweo, aina nyingi za mboga huwa na wingi wa Vitamini C, Carotene, ambayo hatimaye hubadilishwa kuwa Vitamin A, Calcium, chuma pamoja na madini mengine.
Mboga ni jina litumikalo kwa aina nyingi za mimea itumiwayo na binadamu kama chakula au kutowelea chakula kingine. Mboga hizo huwekwa katika makundi matano, yaani:


1. Matunda (nyanya, bilinganya, bamia, matango, pilipili na maharage).
2. Majani (kabeji, letusi, seleri, mchicha na mlenda)
3. Mizizi (karoti, radishi na tanipu)
4. Mashina (vitunguu maji, vitunguu saumu na iliki)
5. Maua (koliflawa na brokoli)


Pengine utajiuliza kwa nini usumbuke kulima mboga zako mwenyewe? Zifuatazo ndizo sababu kubwa za kufanya hivyo:

1. Kupata na kutumia mboga zikiwa katika hali ya upya(hazijaanza kuharibika)
2. Ni rahisi, yaani gharama ya kuzistawisha ni ndogo ukilinganisha na bei ya kuzinunua. Isitoshe aina nyingine za mboga huwa na faida mbili, kwa mfano: kunde, maharage na maboga, hutumiwa tunda na majani yake.
3. Raha ya kufanikiwa; tabia ya binadamu ni kufurahia matunda mazuri ya jasho lake, kwani binadamu hupata uradhi kwa kufanya kazi yake mwenyewe na kufanikiwa.

Baada ya mkulima kuamua kustawisha mboga katika bustani yake mwenyewe, yabidi pia ajiweke katika hali ya kupata mavuno mengi iwezekanavyo. Jambo hili linaweza kutimizwa kwa kuzingatia yafuatayo:
a) Kujua aina ya mboga ziwezazo kustawi vizuri kwa kulingana na mazingira yaliyopo, hasa hali ya hewa na udongo.
b) Kujua muda zichukuao hadi kukomaa kusudi mpango wa kufuatisha nyingine ufanywe mapema.
c) Kufahamu aina na kiasi cha mbolea zinazohitajika kutumiwa, na kufanya mipango ya kuipata wakati inapotakiwa.
d) Kufahamu magonjwa na wadudu washambuliao mboga katika eneo lake(mkulima) analo ishi, na kujua jinsi ya kupambana nao.


Ulimaji wa mboga unaweza ukawekwa katika makundi mawili; bustani ndogo ndogo karibu na makazi yetu, na mashamba makubwa kwa ajili ya biashara. 
Leo nakomea hapa.
(ii) BILINGANYA
Zao hili hustawi zaidi katika nchi za joto, hasa kusini mwa Asia, Mashariki ya Mbali na Afrika.
(a) AINA ZAKE
Kama ilivyo kwa mazao mengine, ziko aina nyingi za bilinganya ambazo hutambuliwa kwa tofauti za maumbile, sura na rangi na hujulikana kwa majina mbali mbali. Aina zinazojulikana zaidi ni: Black Beauty na Early Purple, ambazo ni za mviringo na: Florida High na Sadohara Purple, ambazo ni ndefu nyembamba.

(b) HALI YA HEWA
Bilinganya ni mmea uchukuao muda mrefu kukua, na hauna nguvu nyingi. Huhitaji hali ya joto katika muda wote wa kustawi. Baridi kali huweza kudumaza na pengine kuua mmea.

(c) HALI YA UDONGO
Zao hili huhitaji udongo laini na unyevu wa wastani. Ardhi iwe na rutuba ya kutosha, na kila inapowezekana ni bora kutumia samadi au mbolea ya takataka. Utayarishaji wa ardhi na bustani ni kama vile kwa mazao mengine ya mboga.

(d) KUPANDA NA KUTUNZA.
Kwa kawaida mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma 8 hadi 10. Kisha miche hung'olewa na kupandikizwa kwenye bustani. 
Umbali wa kupanda miche ni sentimeta 60 hadi 90 kati ya mmea, na sentimeta 90 hadi 120 kati ya mistari. Unatakiwa kutifuatifua udongo wa juu mara kwa mara na kila inapolazimika uongezaji wa maji licha ya kutegemea mvua.

(e) MAGONJWA
Kuna magonjwa makubwa mawili ya zao hili, nayo ni:
Fruit Rot: Ugonjwa huu husababishwa na vimelea na hushambulia sehemu zote za mmea isipokuwa mizizi. Majani huwa na madoa ya hudhurungi. Mashina (hasa ya miche michanga) hushambuliwa, na mara nyingi huoza. Matunda nayo hupata madoa hatimaye sehemu zenye athari hiyo hulainika na kuoza. Hakuna dawa maalum ya kuzuia, inashauriwa kubadilisha mpando na kupanda aina zenye uvumilivu.
Wilt: Dalili za ugonjwa huu ni kwamba rangi ya majani hugeuka njano, halafu hupukutika kidogo kidogo. Mimea hudumaa na kufa kabla ya kukomaa

(f)WADUDU
1. Beetles na Aphids- huathiri mimea michanga
2. Lacebug- hufyonza utomvu wa mmea
Kwa wadudu hawa wote, tumia sumu yoyote kama Malathion 5%, Thiodane n.k

Bilinganya husaidia kulainisha usingizi.