Sunday, March 8, 2015

SHUBIRI MWITU (ALOE) TIBA YA MAGONJWA YA KUKU

Shubiri mwitu (Aloe) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa kutmia mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonyesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani.
Picha ya mmea wa Shubiri mwitu. Mmea huu unaweza kupandwa nyumbani kama ua kwenye ndoo au kupandwa ardhini kama mimea mingine.
Maji maji ya mmea huu yanauwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.Mmea wa aloe vera unaweza kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake na unakubali maeneo karibu yote.Majina ya mmea huu kulingana na baadhi ya makabila na kimataifa

Jina la Mmea
Lugha
Shubiri mwitu
Kiswahili
Mkankiruri
Kinyaturu
Itembwe
Kigogo
Ibhata
Kinyiha
Litembwetembwe
Kihehe
Koli
Kikaguru/Kinguu
Aloe
Kiingereza
Aloe vera
Kisayansi

Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kukuKulingana na tafiti zilizofanywa na Bejar (Chuo kikuu cha Kilimo na Misitu cha Samar) na Clapo (Chuo Kikuu cha Ufilipino Mashariki) inaonyesha kuwa ziada ya Shubiri mwitu kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka. Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yanauwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na kuongeza uzito wa ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.Uandaaji wa Shubiri mwitu Kunjwa: Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3 kutegemeana na idadi ya kuku. Viache humo kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama unakuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.
Vidonda:Kuku wenye vidonda kama kwa ugonjwa wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na kuvichekecha ili upate unga laini. Uanike na kisha tunza vizuri tayari kwa kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye vidonda hivyo.

1 comment: