Thursday, March 12, 2015

Wakazi wa MTUMBA wauza mashamba yao kwa wachimba mchanga


Wakazi wa vijiji vya MTUMBA na IHUMWA vilivyopo katika Manispaa ya DODOMA wameamua kugeuza mashamba yao kuwa vitega uchumi kwa kuwauzia wafanyabiashara wa kuchimba mchanga. 

Mbali ya shughuli hiyo ya kuchimba mchanga kuathiri mazao yakiwemo yale ya chakula, pia inatishia uharibifu wa mazingira. 

Mkoa wa Dodoma unaopata mvua chache za msimu, ambazo kwa kiasi kikubwa huathiri pato la mkulima kutokana na kutokuwa na mavuno ya kutosha. 

Baadhi ya wafanyabiashara wa mchanga wamekiri kuchimba mchanga kwenye mashamba ya watu wakidai kupata vibali na leseni kutoka wizara ya Nishati na Madini pia wanadai kuwepo kwa mkanganyiko baina ya manispaa na wizara ya nishati na madini kuhusu vibali. 

Pamoja na katazo la kuchimba mchanga kwenye mashambani ,bado manispaa imeendelea kutoza shilingi elfu kumi kama ushuru wa mapato kwa kila lori la mchanga,hata hivyo wanakiri kuwepo kwa athari.

No comments:

Post a Comment