Wednesday, March 11, 2015

Watu wasiojulikana wachoma shamba la muwekezaji mkoani MANYARA


WATU wasiofahamika wamechoma moto na kuteketeza mali za mwekezaji wa Shamba la HAMIRE ESTATE, lililoko katika eneo la Bonde la KIRUSIX wilayani BABATI mkoani MANYARA, usiku wa kuamkia tarehe 09 March, 2015 
Mali zilizoteketea ni pamoja na Matrekta matatu na nyumba moja iliyokuwa ikitumiwa kama ofisi katika eneo la Mwekezaji huyo 
Tukio hilo litawaweka kando na kazi au kibarua zaidi ya wafanyakazi 200 
waliokuwa wakitegemea kipato chao kila mwezi kwa kufanya kazi katika shamba hilo 
Baadhi ya wenyeji wa eneo hilo akiwemo diwani wa kata ya KIRU, FABIANO TLANKA, wamelaani matukio hayo ya uchomaji moto mali za wawekezaji 
Mbunge wa BABATI VIJIJINI, JITU SONI, ameitaka serikali kudhibiti vitendo hivyo vinavyotishia usalama wa wawekezaji walioko katika Bonde hilo 
Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Mkoani MANYARA, JUSTINE MASEJO, amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linachunguza kuhusu tukio hilo 

No comments:

Post a Comment