Na Josephine Mwaiswaga,
Dar es salaam.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza kushuka kwa kasi ya Mfumuko wa Bei iliyojitokeza kwenye Bidhaa mbalimbali katika mwezi Desemba mwaka jana ambao ulikuwa asilimia 4.8 hadi kufikia asilimia 4.0 kwa Mwezi Januari mwaka huu.
Mkurugenzi wa takwimu za idadi za watu na huduma za kijamii Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumko wa bei hizo kumetokana na kushuka kwa kasi kwa bei za bidhaa za vyakula, Unga, mafuta ya taa Deseli na Petroli.
Akianisha mwenendo wa kupungua kwa bidhaa mbalimbali katika kipindi cha Mwezi Januari Mwaka huu, Kwesigabo amesema bei za mahindi zimepungua kwa asilimia 13.3, unga wa mahindi asilimia 6.2 , Samaki asilimia 7.9 ndizi za kupika asilimia 11.3 na mihogo asilimia 12.0.
Aidha ofisi hiyo ya takwimu imeanishwa kuwa mafuta ya taa yameshuka kwa asilimia 8.4,dizel asilimia 10.2, Petrol asilimia 6.8 wakati gasi ya kupikia imeshuka kwa asilimia 2.1
Aidha, Ofisi hiyo ya pia ikaanisha hali ya mwenendo wa bei katika Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
Mbali na kupungua kwa kasi ya mfumko wa bei katika bidhaa zilianishwa, ofisi hiyo imeainisha kuwa bidhaa za mchele, nyama, lishe ya watoto na mbogambogo bado zimeonekana kuwa juu
No comments:
Post a Comment