Wakulima zaidi ya 2,700 wa mikoa ya NJOMBE, IRINGA na MBEYA, wameanza kunufaika na Mradi wa Uzalishaji wa mbegu za kisasa za viazi Mviringo, Mradi ambao unatekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole kwa kushirikiana na na serikali ya Finland.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Dkt. ZAKARIA MALLE, amesema mradi huo wa miaka Mitatu tayari umefanya utafiti na kugundua mbegu Nne za aina za Viazi Mviringo ambazo zinastahimili magonjwa ukilinganisha na mbeguu zilizoletwa na wakoloni ambazo hazina tija kwa wakulima.
Zao la Viazi Mviringo linastawi kwa wingi katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa, tayari wakulima zaidi ya 2,700 wa wilaya za Kilolo, Mufindi, Waking’ombe,Njombe na ,Mbeya wamenufaika na mradi wa uzalishaji wa Mbegu bora za kisasa za viazi mviringo.
Uboreshaji wa kilimo cha viazi mviringo, ni mpango wa wizara ya kilimo chakula na ushirika kumwezesha mkulima kuwa na uzalishaji wenye tija kuuza viazi ndani na nje ya mipaka ya nchi.
No comments:
Post a Comment