Saturday, February 28, 2015
NG'OMBE JAMII YA ANKOLE
Friday, February 27, 2015
Matrekta 3000 kuingizwa nchini
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO
KAMPUNI ya kutengeneza Matrekta iitwayo ARSUS ya nchini POLAND, inatarajia kuingiza Matrekta elfu tatu (3,000) kwa kushirikiana na kampuni ya SUMA JKT ili kukuza sekta ya kilimo hapa nchini
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO ameiambia TBC mjini BERLIN UJERUMANI, kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya kilimo, ni matokeo ya kuvutia uwekezaji wa eknolojia na mitaji kutoka nje unaofanywa kupitia uwakilishi wa diplomasia ya kiuchumi
Sekta ya kilimo nchini Tanzania inaajiri zaidi ya asilimia 85 ya watanzania hususani waishio vijijini.
Changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni pamoja na matumizi duni ya zana za kilimo hali iliyoifanya Tanzania kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuimarisha sekta hiyo.
Akizungumzia sekta ya utalii, BALOZI PHILIP MARMO amesema kuwa idadi ya watalii kutoka nchi za Ulaya wanaotembelea Tanzania imeongezeka hadi kufikia wastani wa watalii laki nne kila mwaka
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na rais Dokta JAKAYA KIKWETE, imekuwa ikisisitiza mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje kuimarisha utendaji wao wa kazi kwa kuendeleza diplomasia ya kiuchumi badala ya uwakilishi wa kisiasa pekee ili kukuza uchumi wa nchi
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO ameiambia TBC mjini BERLIN UJERUMANI, kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya kilimo, ni matokeo ya kuvutia uwekezaji wa eknolojia na mitaji kutoka nje unaofanywa kupitia uwakilishi wa diplomasia ya kiuchumi
Sekta ya kilimo nchini Tanzania inaajiri zaidi ya asilimia 85 ya watanzania hususani waishio vijijini.
Changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni pamoja na matumizi duni ya zana za kilimo hali iliyoifanya Tanzania kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuimarisha sekta hiyo.
Akizungumzia sekta ya utalii, BALOZI PHILIP MARMO amesema kuwa idadi ya watalii kutoka nchi za Ulaya wanaotembelea Tanzania imeongezeka hadi kufikia wastani wa watalii laki nne kila mwaka
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na rais Dokta JAKAYA KIKWETE, imekuwa ikisisitiza mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje kuimarisha utendaji wao wa kazi kwa kuendeleza diplomasia ya kiuchumi badala ya uwakilishi wa kisiasa pekee ili kukuza uchumi wa nchi
COCA-COLA YAZINDUA UPYA MAJI YA DASANI
Kutoka kushoto ni Meneja wa Coca- Cola, Yebeital Getachew, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios, Meneja Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Hettiarachchi na Msimamizi wa Masoko Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa wakionyesha muonekano mpya wa chupa ya maji ya Dasani baada wakati wa uzinduzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuzindua upya maji ya Dasani.
Chupa ya Dasani inavyoonekana baada ya kuzindua upya maji ya Dasani.
Maji ya Dasani.
Wanamuziki wa bendi ya Odama THT wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano wa Chupa mpya ya maji ya Dasani jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios akizungumza wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya maji ya Dasani katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo.
Wageni waalikwa.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Muonekano wa maji ya Dasani katika chupa mpya.
Wanamuziki wa bendi ya Odama THT wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano wa Chupa mpya ya maji ya Dasani jijini Dar es Salaam.
Wakulima wadogo wabadili mwelekeo wao wa kilimo
SIMU za mkononi ni muhimu zaidi hivi sasa kwa wakulima katika wilaya za Mbeya, Mbarali na Morogoro baada ya kuanza kuzitumia kupata taarifa mbalimbali za masuala ya kilimo.
Matumizi hayo ya wakulima kwa baadhi ya vijiji katika wilaya hizo yanabainisha kuwapo kwa mahitaji ya vipindi vya kilimo katika vyombo vya habari nchini, kutokana na uwepo wa wafuatiliaji wa karibu kwa vipindi hivyo.
Katika baadhi ya vijiji ndani ya wilaya hizo tatu, wakulima hufuatilia vipindi vya kilimo vinavyotolewa katika redio maalumu walizochagua na hutumia simu za mkononi kuwasiliana na waendeshaji vipindi hivyo au wataalamu wao wa kilimo kwa ajili ya kupata taarifa za kilimo anazozihitaji.
Farm radio ni vipindi vinavyorushwa redioni kupitia mradi maalumu wa kuwajengea uwezo wagani katika kuendeleza matumizi ya mikunde kurutubisha udongo nchini, unaotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA).
Kupitia mradi huo, baada ya wagani hao kupatiwa taaluma ya kurutubisha udongo huisambaza kwa wakulima katika maeneo yao kupitia vipindi vya redio na simu za mkononi na kisha, wakulima nao hupata nafasi kuwasiliana na wataalamu hao kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo kupitia vyombo hivyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Mradi huo, Christopher Mkondya, wakulima 260 kutoka vijiji vya Nsongwi, Ifiga na Nsongwi Juu, katika Wilaya ya Mbeya Vijijini wameunganishwa na redio ya Baraka FM kupitia vikundi vyao vya wasikilizaji, na kwa Wilaya ya Mbarali wakulima 160 wameunganishwa na redio Bomba FM.
Wilayani Mbarali, mradi huo unafanya kazi na wakulima waliojiunga katika vikundi vya skimu za umwangiliaji kwa ajili ya kilimo cha mpunga, ambazo ni pamoja na Majengo, Maendeleo na Ruanda Manjenje, ambazo zinahudumia vikundi vya Majengo, Hamasa, Maendeleo na Ruanda Manjenje.
Mbali ya Mbeya, mradi huo pia unahudumia wakulima 160 katika Wilaya ya Kilosa wanaounganishwa na redio ya Aboud FM. Wakulima hao ni kutoka kwenye vijiji vya Kondoa, Chanzuru na Ludewa.
Hata hivyo, wakulima walioko kwenye masafa ya redio hizo nao wamekuwa wakifuatilia, na hivi sasa mahitaji yanaongezeka kwa kasi ambapo wakulima wengi zaidi kutoka vijiji visivyofikiwa na huduma hiyo, wanashinikiza kuingizwa kwenye mradi ili nao wanufaike na elimu ya kilimo bora inayotolewa kupitia vifaa hivyo vya elekroniki.
“Mwitikio wa wakulima ni nzuri, wanashirikishwa katika vipindi, hujisajili kwenye orodha ya simu ili kupata taarifa mpya za vipindi na taarifa za kilimo,” anasema Mkurugenzi wa Baraka FM, Henry Mazunda.
Watayarishaji wa vipindi hivyo wanathibitisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya taarifa za kilimo, ambapo wakulima wenye kubahatika kunasa mawimbi ya vipindi hivyo huwapigia simu kuomba kushirikishwa kwenye mpango huo pamoja na kupatiwa elimu ya mazao mengine zaidi ya mahindi na yale ya jamii ya mikunde.
“Wakulima wengi zaidi kutoka nje ya mradi wanafuatilia na kuuliza maswali, nao wanataka kushirikishwa kwenye mradi,” anasema Lina Mwambungu, mmoja wa watayarishaji wa vipindi hivyo vya wakulima.
Lina anazitaja taarifa zinazopatikana kupitia ujumbe mfupi wa simu kuwa ni pamoja kukumbushwa siku na muda wa kipindi, elimu kuhusu kilimo bora cha mahindi na mazao jamii ya mikunde, wakulima hutuma maswali kuhusu taarifa wanazohitaji au maombi ya kurudiwa kwa kipindi.
Ofisa ugani kutoka Kijiji cha Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Abubakar Ramadhan anauona mradi huo kuwa wenye tija kwa wakulima na kubainisha kuwa kwa mkulima mwenye kushiriki kikamilifu kwenye mradi huo huongeza wingi na ubora wa mazao yake.
Anasema shamba lenye mchanganyiko wa mahindi na mikunde huongeza tija katika uzalishaji kutokana na virutubisho vinavyotengezwa na mazao jamii ya mikunde na wakati huo huo hutunza udongo, hauchakai na kupoteza uwezo wake wa kuzalisha.
Katika msimu wa kilimo wa 2012/2013, mkulima kutoka Kikundi Faida Mwandaji, Jela Mandewela alikuwa na ekari moja ya kilimo mseto ambapo alipanda mahindi na maharage, na katika mavuno yake amevuna maharage kilo 300, mahindi ikiwa ni kati ya gunia 22 hadi 26.
Hali hiyo anasema ni tofauti na huko nyuma alipovuna gunia kati ya tatu na saba katika ekari ile ile moja, na wakati huo huo akikosa maharage ambayo alilazimika kuyalima kwenye eneo jingine hivyo kutokuwa na matumizi mazuri ya ardhi.
“Tunapata elimu kutoka kwa ofisa ugavi na vipindi vya redio, tunarekodi mambo yetu ya kilimo, tunatumia simu kuwasiliana na wataalamu wetu na watangazaji,” anasema Mandewele kisha anaongeza akisema; “redio inatusaidi kupata elimu, tunatambulika na watu, wanatusikiliza.”
Rozina Mohamed kutoka Kijiji hicho cha Mantanji anakielezea kilimo mseto kuwa na faida zaidi kwao ambapo anasema tangu aingie kwenye kilimo hicho ameweza kuongeza kipato cha familia yake na sasa anamudu kusomesha watoto wake walioko shule za sekondari.
Manufaa mengine aliyopata ni pamoja na kuezeka bati kwenye nyumba yake, kuweka maji ya bomba na amenunua mifugo ikiwemo ng’ombe na mbuzi, akisisitiza kwamba kilimo kina faida kuliko uchuuzi.
Hata hivyo mradi huo unakabiliwa na changamoto kubwa ya mahitaji kuzidi uwezo uliopo sasa. Mradi unaelekeza darasa moja la maofisa ugani kuwa na watu 40 kwa chuo, lakini kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji wamejikuta wakifika hadi 70 lakini wakihudumiwa na rasilimali zile zile za watu 40.
Vyuo vinavyohusika na utoaji elimu hiyo kwa wagani ni MATI Uyole na Igurusi vilivyopo mkoani Mbeya na kile cha Ilonga mkoani Morogoro.
Katika mfumo wa uendeshaji mradi huo, kila chuo kimekuwa kikihudumia vijiji vitatu vinavyokizunguka na kwamba ni wakulima wenyewe ambao huchagua redio ambazo wangependa zitumike kuwarushia matangazo hayo.
Mkondya anasema, uandaaji wa vipindi hivyo hufanywa kwa kushirikiana kati ya wakulima, wagani na watangazaji ambao huwatembelea wakulima kwenye vijiji vyao na kuandaa nao vipindi.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/wakulima-wadogo-wabadili-mwelekeo-wao-wa-kilimo#sthash.O55W8xaH.dpuf
Thursday, February 26, 2015
FAIDA ZA UFUGAJI WA NG'OMBE
FAIDA ZA UFUGAJI WA NG'OMBE
Ufugaji wa ng'ombe umekuwa ukifanywa tangu enzi za mababu zetu na haiwahi tokea mfugaji kujua kwa nini anafanya ufugaji. Sababu kubwa ni faida ziletwazo na ufugaji, ng'ombe kwa mfano amekuwa akimletea mfugaji faida zifuatazo:
1. Hutoa Nyama
Nyama ya ng'ombe ni chanzo kizuri cha protini kwa binadamu na kila siku duniani kote huchinjwa nyama ya ng'ombe na huliwa na asilimia kubwa sana ya binadamu duniani. Mabucha mengi makubwa duniani ni kwa ajili ya uchinjaji wa ng'ombe na pengine ndo mabucha ya kwanza kuanzishwa. Hapa Tanzania machinjio yote makubwa ni kwa ajili ya ng'ombe. Hii inaonyesha namna gani nyama ya ng'ombe huhitajika na binadamu.
Nyama ya ng'ombe ikiwa imening'inizwa |
Banda bora la kufugia ndama
KILIMO KWANZA: KILIMO CHA KUTUMIA JEMBE LA KUKOKOTWA NA NG'OMBE
Wakulima wa kahawa KAGERA washauriwa kujiunga vyama vya ushirika
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya MULEBA Mkoani KAGERA limeshauri wakulima wa zao la kahawa wilayani humo kujiengua kutoka katika Chama cha Ushirika mkoani KAGERA (KCU), na kuunda ushirika wao.
Katika kikao hicho baadhi ya madiwani wamesema KCU hakijafanya jitihada za kumkomboa mkulima, ikiwa ni pamoja na kumpatia bei nzuri hususani ya zao la kahawa na hivyo kusababisha mkulima kujitafutia masoko nje ya nchi ili kujipatia unafuu wa bei.
Azimio hilo limetokana na na taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa mbele ya madiwani hao na Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo GEORGE KATOMERO , kuwa halmshauri hiyo imeshindwa kukusanya asilimia hamsini ya mapato ya ndani kama makisio ya nusu mwaka, kutokana na sababu kadhaa ikiwemo usafirishwaji wa magendo ya kahawa nje ya nchi.
Hoja ya njia ipi itumike kuzuia magendo ya kahawa ikawasilishwa na baadhi ya madiwani ,wengi wao wakidai sababu kubwa ni bei ya chini inayotolewa na Chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera (KCU)
Katika mkutano Mkuu wa Chama cha ushirika mkoani Kagera (KCU) Mwenyekiti wa Chama hicho FRANK MUGANYIZI amekiri kuwepo kwa bei ndogo katika soko la kahawa ,lakini Mkuu wa Mkoa wa Kagera JOHN MONGELLA akitoa ilani kwa wale wote wanaojihusisha na biashara ya magendo ya kahawa kuwa mkono wa sheria itawakabili.
Licha ya Hivi karibuni Chama cha Msingi MAGATA KURUTANGA kilichopo wilayani MULEBA, kujiondoa kutoka chama kikuu cha ushirika mkoani KAGERA (KCU)Madiwani hao wanataka kuwepo na muundo wa chama kikubwa cha ushirika kitakachojumuisha wakulima wote kutoka katika wilaya hiyo.
Katika kikao hicho baadhi ya madiwani wamesema KCU hakijafanya jitihada za kumkomboa mkulima, ikiwa ni pamoja na kumpatia bei nzuri hususani ya zao la kahawa na hivyo kusababisha mkulima kujitafutia masoko nje ya nchi ili kujipatia unafuu wa bei.
Azimio hilo limetokana na na taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa mbele ya madiwani hao na Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo GEORGE KATOMERO , kuwa halmshauri hiyo imeshindwa kukusanya asilimia hamsini ya mapato ya ndani kama makisio ya nusu mwaka, kutokana na sababu kadhaa ikiwemo usafirishwaji wa magendo ya kahawa nje ya nchi.
Hoja ya njia ipi itumike kuzuia magendo ya kahawa ikawasilishwa na baadhi ya madiwani ,wengi wao wakidai sababu kubwa ni bei ya chini inayotolewa na Chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera (KCU)
Katika mkutano Mkuu wa Chama cha ushirika mkoani Kagera (KCU) Mwenyekiti wa Chama hicho FRANK MUGANYIZI amekiri kuwepo kwa bei ndogo katika soko la kahawa ,lakini Mkuu wa Mkoa wa Kagera JOHN MONGELLA akitoa ilani kwa wale wote wanaojihusisha na biashara ya magendo ya kahawa kuwa mkono wa sheria itawakabili.
Licha ya Hivi karibuni Chama cha Msingi MAGATA KURUTANGA kilichopo wilayani MULEBA, kujiondoa kutoka chama kikuu cha ushirika mkoani KAGERA (KCU)Madiwani hao wanataka kuwepo na muundo wa chama kikubwa cha ushirika kitakachojumuisha wakulima wote kutoka katika wilaya hiyo.
Serikali yatenga Sh. Bil. 30 kuwalipa wakulima.
Na Mkombe Zanda,
Mbeya.
Serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwalipa wakulima waliouza mazao yao kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema fedha hizo zitalipwa kwa Wakulima katika awamu mbili za shilingi bilioni 15 ili kumaliza malalamiko yanayotokana na kuchelewa kwa malipo hayo.
Hayo yalibainishwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, katika siku ya kwanza ya ziara ya wiki moja mkoani Mbeya akiwa wilayani Mbarali, ambapo pia alipata fursa kufungua maabara za sayansi katika shule ya sekondari ya Igomelo na kusomewa taarifa ya kazi ya wilaya hiyo.
Katika mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alibainisha kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya kuwalipa wakulima waliouza mazao yao kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, NFRA.
Kuhusu mgogoro wa mpaka unaotenganisha Hifadhi ya Bonde la Ihefu na makazi ya watu wilayani Mbarali, Waziri Mkuu amesema Serikali itapitia upya sheria ndogo inayohusu mpaka huo ili kuondoa kasoro zilizopo.
Katika kukabiliana na uhaba wa Walimu wa Sayansi, Pinda, alisema Serikali imeongeza ajira za wakulimu hao.
Hii ni ziara ya kwanza kwa Waziri Mkuu Pinda mkoani Mbeya kwa mwaka huu.
UFUGAJI KWA UJUMLA
Ufugaji : ni neno linalotumika kumaanisha wanyama wanaofugwa na binadamu kwa malengo ya kumpatia chakula au faida Fulani. Mifugo inaweza kufugwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji madogo madogo au ufugaji wa faida wenye kuinua uchumi wa mfugaji. Wanyama wanaoweza kufugwa na binadamu ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na aina zake, njiwa, punda, farasi, kware, kanga, ngamia, na mbogo maji. Mbwa nap aka hufugwa na binadamu kwa ajili ya kumsaidia ulinzi lakini pia siku hizi hufugwa kama rafiki wa binadamu
MADHUMUNI YA UFUGAJIYapo madhumuni makubwa mawili yanayoweza kumvuta mtu fulani apende kufuga;
a) Thamani ya kiuchumi itokanayo na ufugajii. Nyama- Nyama ni muhimu kwa ajili ya kupata protini na nguvu, mfugaji akiuza nyama au mfugo wenyewe ukiwa mzima anajipatia kipato.ii. Maziwa na mazao yake- Kut okana na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia na mbogo maji, mfugaji anaweza kujipatia maziwa na mazao yake kama mtindi, jibini, na siagi/samuli. Maziwa na mazao haya anaweza kuyatumia katka familia lakini pia akauza kujiongezea kipato chake.iii. Nyuzi- baadhi ya mifugo manyoa yake yanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali kama kutengenezea nguo mfano manyoa ya kuku, mbuzi, kondoo, ng’ombe. Hivyo yakiuzwa yanasaidia kuongeza kipato.iv. Mifupa, pembe na Ngozi- Ngozi ya mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo hutumika kutengeneza viatu, nguo. Mifupa hutumika kutengenezea viatu, gundi, kuwambia ngoma, na chakula cha mifugo, wakati pembe hutumika kwa mabaragumu yanayopigwa kwenye ngoma za jadi, kutoa taarifa fulani katika jamii.v. Mbolea ya mifugo- Hutumika mashambani kuongeza uzalishaji, kukandikia nyumba, kuchomea matofali na vyungu, pia hutumika kama kuni, na kuzalishia gesi. Mbolea inaweza ikauzwa na kumpatia mfugaji pesa kwa matumizi yake mbalmbali.vi. Nguvu kazi-Mifugo mingi hutumiwa na binadamu kumsaidia kufanya kazi ulani, mfano ngombe na punda hutumika kwa ajili ya kulima, kukota mikokoteni, kuvuta miti na mizigo mingine. Punda, farasi na ngamia hutumika kama usafiri wa kusafisha watu au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine au wakati mfugaji anahama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.
b) Thamani isiyo ya kiuchumii. Ufahari- Kuwa na mifugo kunamletea mfugaji ufahari na hivyo kumfanya awe na amani kwani hana hofu hata akiwa na matatizo anayosehemu ya kukimbilia kwa haraka bila ya kupata msongo wa mawazo.ii. Kuwa sehemu ya familia- Wapo watu wanaofuga wanyama kwa lengo la kuwa marafiki wa karibu au kuwa sehemu ya familia, wanyama wanaofugwa kwa jinsi hii hawauzwi wala hawaliwi. Tena mnyama akiugua au kufa huduma yake inafanana sana ya mwanadamu mwenye mfugo hupata huzuni.iii. Imani ya kidini- Wapo wanaofuga wanya kwa lengo la kuabudu kama miungu wao, mfano dini ya kihindi huabudu ng’ombe. Lakini pia mifugo hutumika kwenye imani za kimila wanapofanya matambiko au kutoa kafara kwa waganga wa kienyeji au wanapofanya mazindiko ya mali, mashamba, nyumba, au magari. Wanya wamekuwa wakitumika kwa kazi hii tangu karne nyingi zilizopiata.iv. Kusafisha mashamba- Mifugo pia hutumika kwa lengo la kusafisha mashamba kwa kulishia mifugo kwenye mashamba ili yawe safi. Wakati mifugo inakula nyasi na majani ya shamba pamoja na kukanyaga huasidia kuua magugu na kuzuia yasiote. Njia hii si nzuri kwa upande mwingine kwa vile huharibu pia virutubisho vya shamba na kufanya litoe mazao duni.
AINA ZA UFUGAJIZipo aina kuu mbili za ufugaji, ufugaji wa kuhamahama na ufugaji wa kutulia eneo moja. Wafugaji wa jamii ya kuhamahama huhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa lengo la kuatafuta chakula, maji na kukimbia magonjwa ya mifugo. Uhamaji huu hutegemea kipindi cha mwaka, wakati wa mvua wafugaji husogea karibu na sehemu ambapo kuna makazi ya kudumu ya watu wengine kwa ajili ya urahisi wa mahitaji mengine ya kijamii. Wakati wa mvua huwa hakuna shida ya maji na chakula maeneo mengi. Wakati wa kiangazi maeneo haya majani huwa yameisha nap engine maji hakuna, hivyo huhama kwenda sehemu ambapo watapata mahitaji hayo. Ufugaji wa aina hii hufanywa kwa ng’ombe wa kienyeji tu kwani ndio wanaoweza kuvumilia joto, magonjwa na shuruti nyingine nyingi zinazopatikana wakati wa uhamaji. Wafugaji wanaofanya ufugaji huu ni wa jamii ya kimasai, kisukuma, na kibarbeiji, hawa wameshazoea kuishi porini na hawanatabia ya kujenga makazi ya kudumu kwa sababu ya kuhamahama. Hasara kubwa ya ufugaji huu ni kukosa huduma za msingi kama shule, hospitali, makanisa na misikiti. Lakini kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la watu linalofanya maeneo ya kulishia kupungua kunafanya wafugaji hawa sasa wanze kuhama kutoka aina hii ya ufugaji kuingia ile ya kutokuhamahama.Ufugaji usio wa kuhamaha unafanywa na watu wanaoishi sehemu moja kama kijiji na kufanya ufugaji wao ndani ya jamii. Hawa hufuga mifugo yao kwa kuifungia ndani muda wote na kuwaletea majani au kwa kuwachunga mchana na jioni kuwafungia ndani. Wale wanaowafungia ndani wanahitaji wakati mwingine kulima majani yatakayotumika kuwalisha mifugo yao. Hapa ufuagaji wa kisasa na wa kienyeji hufanyika kwa njia zote mbili, kuwafungia ndani muda wote au usiku tu. Huu ndiyo ufugaji wenye tija, kwani mfugaji atakuwa na mifugo michache na ataihudumia kirahisi zaidi kwa kuwapa huduma zinazotakiwa.
Washindi wa Promesheni ya Airtel yatosha Zaidi wakabithiwa magari yao
Washindi wa Promesheni ya Airtel yatosha Zaidi wakabithiwa magari yao
Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (katikati) akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Kondakta wa Malori, Jastini William Dodoo katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo akiwa mwenye furaha ndani ya gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, baada ya kukabidhiwa na Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (kushoto), katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kulia), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa mshindi huyo, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi kadi ya umiliki wa gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (wa pili kushoto) ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akiteremka kutoka kwenye gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 464 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Wakala wa Mtandao huo, John Fred Kiwale katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Togo, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na (kulia) ni Mke wa mshindi huyo, Anna Kiwale na motto wake, Sylvia John.
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (katikati), akifafanua jambo kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo (kulia), baada ya kumkabidhi gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
Wakazi wa arusha wahimizwa kulima mazao yanayohimili ukame
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA,FELIX NTIBENDA
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA,FELIX NTIBENDA amewaagiza wakazi wa wilaya ya ARUMERU mkoani ARUSHA,kulima mazao yanayostahimili ukame ili kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula unajitokeza kutokana na uhaba wa mvua.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha Halmashauri ya MERU,mkuu wa mkoa amesema kuanzia sasa hakuna maafisa kilimo kukaa ofisini na badala yake watembelee mashamba ya wakulima ili kuona tatizo linalowakabili katika kilimo.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha Halmashauri ya MERU,mkuu wa mkoa amesema kuanzia sasa hakuna maafisa kilimo kukaa ofisini na badala yake watembelee mashamba ya wakulima ili kuona tatizo linalowakabili katika kilimo.
Wednesday, February 25, 2015
Tanzania yaweka mipango ya kuwainua wafugaji nyuki
Dakta ANACLETI KASHULIZA
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi – NEEC Dakta ANACLETI KASHULIZA amesema kuwa TANZANIA imeweka malengo SITA yenye lengo la kuwainua wafugaji nyuki nchini katika maeneo ya mijini na vijijini ili waweze kuzalisha asali yenye kiwango kinachokubalika kimataifa.
Dakta KASHULIZA ameyasema hayo Jijini ARUSHA wakati wa kongamano la kwanza la ufugaji nyuki katika Bara la AFRIKA linalojumuisha wafugaji nyuki kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa Dakta KASHULIZA, TANZANIA inapaswa kuzalisha asali inayokubalika katika nchi mbalimbali Duniani hususani MAREKANI ambapo hivi sasa wananunua asali kwa wingi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa huduma za misitu nchini JUMA MGOO amesema sera na sheria za umiliki wa misitu zinaruhusu kumiliki maeneo kwa kufuata ngazi zote muhimu ambapo asilimia Arobaini ya mistu inamilikiwa na serikali na asilimia Arobaini na Tano iko chini ya usimamizi wa vijiji.
Dakta KASHULIZA ameyasema hayo Jijini ARUSHA wakati wa kongamano la kwanza la ufugaji nyuki katika Bara la AFRIKA linalojumuisha wafugaji nyuki kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa Dakta KASHULIZA, TANZANIA inapaswa kuzalisha asali inayokubalika katika nchi mbalimbali Duniani hususani MAREKANI ambapo hivi sasa wananunua asali kwa wingi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa huduma za misitu nchini JUMA MGOO amesema sera na sheria za umiliki wa misitu zinaruhusu kumiliki maeneo kwa kufuata ngazi zote muhimu ambapo asilimia Arobaini ya mistu inamilikiwa na serikali na asilimia Arobaini na Tano iko chini ya usimamizi wa vijiji.
Waziri mkuu awasifu wakulima
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesifu juhudi zinazofanywa na wakulima kote nchini kwa kuzalisha chakula kwa wingi na hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na ziada ya chakula.
Waziri Mkuu PINDA ametoa kauli hiyo mkoani MBEYA wakati wa mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa IGAWA wilayani MBARALI muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku NANE.
Katika Ziara yake waziri mkuu ameanzia wilaya ya Mbarali ambapo amezindua maabara katika shule ya sekondari ya Igomelo.
Kutokana na juhudi za wanafunzi hasa wakike, Mke wa Waziri Mkuu Mama TUNU PINDA amehimiza wasichana kutumia fursa iliyopo ya kusoma kwa bidii masomo ya mchepuo wa sayansi kwa kuwa serikali iko nyuma yao.
Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya tayari imekamilisha ujenzi wa maabara kama agizo la rais kwa asilimia 99, kilichobaki ni kemikali pamoja na vitendanishi ndani na maabara hizi.
Pamoja na kusifu juhudi za wananchi wa Mbarali kwa kutekeleza agizo la Rais kwa Vitendo,na kwamba serikali iko katika kuhakikisha inaajiri walimu wa sayansi katika wilaya zilizoitikia kwa wepesi ujenzi wa maabara,Lakini Mtoto wa mkulima hajasita kuwapongeza wakulima kote nchini kwa kuliletea taifa heshima ndani na nje ya mipaka.
Waziri Mkuu PINDA ametoa kauli hiyo mkoani MBEYA wakati wa mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa IGAWA wilayani MBARALI muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku NANE.
Katika Ziara yake waziri mkuu ameanzia wilaya ya Mbarali ambapo amezindua maabara katika shule ya sekondari ya Igomelo.
Kutokana na juhudi za wanafunzi hasa wakike, Mke wa Waziri Mkuu Mama TUNU PINDA amehimiza wasichana kutumia fursa iliyopo ya kusoma kwa bidii masomo ya mchepuo wa sayansi kwa kuwa serikali iko nyuma yao.
Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya tayari imekamilisha ujenzi wa maabara kama agizo la rais kwa asilimia 99, kilichobaki ni kemikali pamoja na vitendanishi ndani na maabara hizi.
Pamoja na kusifu juhudi za wananchi wa Mbarali kwa kutekeleza agizo la Rais kwa Vitendo,na kwamba serikali iko katika kuhakikisha inaajiri walimu wa sayansi katika wilaya zilizoitikia kwa wepesi ujenzi wa maabara,Lakini Mtoto wa mkulima hajasita kuwapongeza wakulima kote nchini kwa kuliletea taifa heshima ndani na nje ya mipaka.
VODACOM NA TIGO WAUNGANA KUTOA HUDUMA BORA ZA KIFEDHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya M-Pesa na Tigo kupitia huduma yake ya Tigopesa. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez.
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya Tigopesa na Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa. Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza.
UGINJWA WA VINUNDU KWA NG'OMBE (LUMPY SKIN DISEASE)
Vinundu vya Lumpy Skin Disease vikiwa vimesambaa mwili mzima |
Dalili za ugonjwa:
-Juto kali la mwili lisilozidi nyuzi joto 41-Vidonda mdomoni na ng'ombe hutoa mate mengi mdomoni-Ute mzito humtoka ng'ombe machoni na puani ambao hufanana na usaha-Kupungua kwa kiasi kikubwa cha maziwa kwa ng'ombe anayekamuliwa-Uwepo wa viuvimbe mwili mzima vinavyompa maumivu ng'ombe. Ukubwa wa viuvimbe hivi ni kati ya sentimita 2 hadi 5 hasa maeneo ya kichwa, shingo na sehemu ya kiwele.-Ng'ombe hudhoofu-Kupungua kwa hamu ya kula-Ng'ombe hukonda-Matezi hasa yaliyopo maeneo ya miguu ya mbele huwa yamevimba sana-Maeneo ya maungio ya miguu huwa yemejaa maji maji na kumfanya ng'ombe atembee kwa shida au kushindwa kutembea kabisa-Ngombe wenye mimba hutupa mimba na mimba iliyotupwa huonekana na viuvimbe hivi kwenye ngozi-Ng'ombe dume anaweza kupata utasa wa kudumu-Ng'ombe wanaweza kupona wenyewe japo taratibu kulingana ukondefu, kichomi, ugonjwa wa kiwele na kiasi cha vidonda vilivyotokana na kupasuka kwa viuvimbe
Matibabu na Uzuiaji
-Hakuna matibabu kamili kwa ugonjwa huu kama kwa magonjwa mengine ya virusi-Dawa (antibiotics) zitatumika ili kuzuia maambukizi pili yanayoweza kuletwa na vijinyemelea vya maongwa mengine kama bakteria-Chanjo kwa ajili ya ugonjwa huu ipo inayoweza kumkinga mnyama kwa muda wa hadi miaka mitatu-Ng'ombe wagonjwa watengwe kutoka wale wazima ili kuzuia maambukizi ya kugusana
Mahitaji ya ng’ombe ili aongeze maziwa
Wape ng’ombe wako lishe kamili, yenye nguvu, protini, na vitamin pamoja na maji ya kutosha.
Kulisha ng’ombe kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa binadamu, ng’ombe anahitaji mlo kamili. Malisho ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo.
Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana. Wanyama wadogo wanahitaji virutubisho vya kutosha, ili wakuwe na kuongeza uzito. Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.
Malisho ya kijani ni mlo mkuu kwa mifugo
Mlo muhimu na wenye virutubisho kwa mifugo ni majani. Lakini malisho bora ya kijani ni yale yanayoweza kumpatia ng’ombe wa maziwa virutubisho muhimu vinavyohitajika. Malisho bora yanakuwa na sifa mbili muhimu: ni ya kijani kibichi na machanga hii ina maana kuwa, majani ya malisho ni lazima yakatwe na kuhifadhiwa yakiwa bado machanga na kabla ya kuchanua. Ni lazima mfugaji afahamu kuwa mimea ambayo imepoteza rangi yake halisi ya kijani inaweza tu kuwasaidia mifugo kuishi lakini haina virutubisho muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, madini, protini na haiwezi kusaidia katika uzalishaji wa maziwa. Malisho yenye viwango vya chini vya virutubisho ni lazima yaongezewe kwa chakula cha ziada chenye virutubisho vya kutosha kitakachoziba pengo la virutubisho vilivyokosekana.
Funza chakula kipya cha mifugo
Je unaweza kula nyama ya mifugo waliolishwa Funza? Kufuga Nguruwe, Kuku, Samaki kwa kuwalisha funza, kunatarajiwa kubadili tunavyo fuga mifugo.
Haya hufanyika katika sehemu moja ya kufanyia majaribio inayomilikiwa na kampunib ya AgriProtein nchini Africa Kusini.
Kampuni hiyo inatengeneza litakalokua shamba kubwa kabisa duniani , linalofuga Nzi. Ufaransa, Kanada, Uholanzi, na Marekani pia wana mipango hiyo.
Mamia ya watu walishiriki kikao cha 'Funza kulisha Ulimwengu' , kilichofanyika huko Wageningen, Uholanzi, mapema mwezi huu.
Wengi waliridhika kuwa Funza na Buu wanaweza kutupa lishe mbadala kwa lishe ile ya kawaida ya Soya na Samaki ambayo yanazidi kuwa ghali.
Shirika la chakula na kilimo duniani linabashiri kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu duniani kutaongeza na mahitaji ya proteni inayotokana na Nyama na Samaki.
Hivyo basi kutakuwa na ushindani kati ya wanyama na binadamu, hususan katika mahitaji ya Proteni.
Kwa upande wa wanyama ongezeko la mahitaji ya proteni litafika asilimia 70 ifikapo mwaka 2050.
Hili litapunguza ardhi inayoweza fanyiwa ukulima na pia hifadhi za Samaki. Vyakula vya Samaki na Ng'ombe vyazidi kuwa ghali. Nafaka hutumika kutupa protini, lakini protini katika mimea haitoshi.
Soya ina protini za kutosha ila tu bei yake imekua ghali.
'Twahitaji vyakula mbadala.'
Aina tofauti ya Nzi, waweza kutumika kutengeza aina tofauti ya vyakula kwa kila hatua ya kukua katika maisha ya mnyama yeyote yule.
AgriProtein ilitangaza kuwa ilikua imekwisha changisha dola milioni 11, kwa matumizi ya ujenzi wa mashamba mawili ya kwanza ya kufuga nzi wa kuuzwa. Shamba la kwanza huko Cape Town litakua na Uwezo wa kutoa tani 20 ya buu na tani 20 za mbolea kila siku.
Wao hutumia aina tatu za Nzi akiwemo Yule wa kawaida wa nyumba, kila aina akiwa na aina tofauti ya vyakula anavyovila. Nzi wa kike na wale wa kiume hufugwa katika vizimba vikubwa na mayai yao kuchukuliwa kisha kuchanganywa na vyakula vyao.
Kilo moja ya mayai yao hugeuka kuwa takriban kilo 380 ya buu, katika muda wa siku tatu tuu. Buu hawa hutolewaa kisha kukaushwa na kusiagwa na kinachobakia hua ni mbolea iliyo na Naitrojini.
Subscribe to:
Posts (Atom)