Wednesday, February 25, 2015

UGINJWA WA VINUNDU KWA NG'OMBE (LUMPY SKIN DISEASE)


Vinundu vya Lumpy Skin Disease vikiwa vimesambaa mwili mzima 
Ni ugonjwa unasababishwa na virusi ukishambulia zaidi ng'ombe, wanyama wengine waanaojulikana kushambuliwa na ugonjwa huu ni pamoja na nyati, swala na twiga

Dalili za ugonjwa:

-Juto kali la mwili lisilozidi nyuzi joto 41-Vidonda mdomoni na ng'ombe hutoa mate mengi mdomoni-Ute mzito humtoka ng'ombe machoni na puani ambao hufanana na usaha-Kupungua kwa kiasi kikubwa cha maziwa kwa ng'ombe anayekamuliwa-Uwepo wa viuvimbe mwili mzima vinavyompa maumivu ng'ombe. Ukubwa wa viuvimbe hivi ni kati ya sentimita 2 hadi 5 hasa maeneo ya kichwa, shingo na sehemu ya kiwele.-Ng'ombe hudhoofu-Kupungua kwa hamu ya kula-Ng'ombe hukonda-Matezi hasa yaliyopo maeneo ya miguu ya mbele huwa yamevimba sana-Maeneo ya maungio ya miguu huwa yemejaa maji maji na kumfanya ng'ombe atembee kwa shida au kushindwa kutembea kabisa-Ngombe wenye mimba hutupa mimba na mimba iliyotupwa huonekana na viuvimbe hivi kwenye ngozi-Ng'ombe dume anaweza kupata utasa wa kudumu-Ng'ombe wanaweza kupona wenyewe japo taratibu kulingana ukondefu, kichomi, ugonjwa wa kiwele na kiasi cha vidonda vilivyotokana na kupasuka kwa viuvimbe

Matibabu na Uzuiaji

-Hakuna matibabu kamili kwa ugonjwa huu kama kwa magonjwa mengine ya virusi-Dawa (antibiotics) zitatumika ili kuzuia maambukizi pili yanayoweza kuletwa na vijinyemelea vya maongwa mengine kama bakteria-Chanjo kwa ajili ya ugonjwa huu ipo inayoweza kumkinga mnyama kwa muda wa hadi miaka mitatu-Ng'ombe wagonjwa watengwe kutoka wale wazima ili kuzuia maambukizi ya kugusana

1 comment: