FAIDA ZA UFUGAJI WA NG'OMBE
Ufugaji wa ng'ombe umekuwa ukifanywa tangu enzi za mababu zetu na haiwahi tokea mfugaji kujua kwa nini anafanya ufugaji. Sababu kubwa ni faida ziletwazo na ufugaji, ng'ombe kwa mfano amekuwa akimletea mfugaji faida zifuatazo:
1. Hutoa Nyama
Nyama ya ng'ombe ni chanzo kizuri cha protini kwa binadamu na kila siku duniani kote huchinjwa nyama ya ng'ombe na huliwa na asilimia kubwa sana ya binadamu duniani. Mabucha mengi makubwa duniani ni kwa ajili ya uchinjaji wa ng'ombe na pengine ndo mabucha ya kwanza kuanzishwa. Hapa Tanzania machinjio yote makubwa ni kwa ajili ya ng'ombe. Hii inaonyesha namna gani nyama ya ng'ombe huhitajika na binadamu.
Nyama ya ng'ombe ikiwa imening'inizwa |
2. Humpatia mfugaji maziwa
Mfugaji anafaidi moja kwa moja maziwa kwa kuyatumia pale nyumbani akiyanwa au akiyatumia kama sehemu ya chakula (mboga). Lakini pia maziwa yamesaidia sana kuinua kipato cha mfugaji hasa anayefuata kanuni za ufugaji kwa kuyauzaa. Hivi sasa soko la maziwa ni kubwa sana kulingana na watu wengi kutambua umuhimu wa kunywa maziwa katika familia zao.
Mfugaji mdogo akikamua maziwa kwa ajili ya matumizi yake nyumbani na mengine kwa ajili ya kuuza |
Moja ya ng'ombe wa maziwa aliyewahi kushiriki kwenye mashindano ya ng'ombe wa maziwa katika maonyesho ya mifugo nane nane Dodoma, nyuma ni mtumishi aliyemuongoza ng'ombe kwenye paredi |
Ng'ombe wamekuwa wakitumika tangu enzi kumurahisishia kazi mwanadamu katika maisha yake. Ng'ombe hutumika kukokota miti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, mazizi ya mifugo na uzio wa nyumba au mashamba. Pia wamekuwa wakitumika kukokota mikokoteni inayokuwa imebeba mizigo (mfano mazao) au watu wakisafiri au kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ng'ombe akikokota mkokoteni uliobeba watu na mizigo |
- 4. Ng'ombe hutumika kwa kilimo
Kilimo cha kutumia ng'ombe |
Mbolea ya samadi hutumiwa na mfugaji na watu wengine kwa ajili ya kurutubisha shamba, kurutubisha miti na wengine hutumia kwa ajili ya kujengea nyumba zao za kuishi (kusiriba kuta au paa).
Kinyesi cha Ng'ombe |
Uyoga pia waweza kuoteshwa kwa kutumia mbolea ya samadi |
- 6. Ng'ombe hutoa zao la ng'ozi
No comments:
Post a Comment