Wednesday, February 25, 2015

Waziri mkuu awasifu wakulima

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesifu juhudi zinazofanywa na wakulima kote nchini kwa kuzalisha chakula kwa wingi na hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na ziada ya chakula.

Waziri Mkuu PINDA ametoa kauli hiyo mkoani MBEYA wakati wa mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa IGAWA wilayani MBARALI muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku NANE.

Katika Ziara yake waziri mkuu ameanzia wilaya ya Mbarali ambapo amezindua maabara katika shule ya sekondari ya Igomelo.

Kutokana na juhudi za wanafunzi hasa wakike, Mke wa Waziri Mkuu Mama TUNU PINDA amehimiza wasichana kutumia fursa iliyopo ya kusoma kwa bidii masomo ya mchepuo wa sayansi kwa kuwa serikali iko nyuma yao.

Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya tayari imekamilisha ujenzi wa maabara kama agizo la rais kwa asilimia 99, kilichobaki ni kemikali pamoja na vitendanishi ndani na maabara hizi.

Pamoja na kusifu juhudi za wananchi wa Mbarali kwa kutekeleza agizo la Rais kwa Vitendo,na kwamba serikali iko katika kuhakikisha inaajiri walimu wa sayansi katika wilaya zilizoitikia kwa wepesi ujenzi wa maabara,Lakini Mtoto wa mkulima hajasita kuwapongeza wakulima kote nchini kwa kuliletea taifa heshima ndani na nje ya mipaka.

No comments:

Post a Comment