Sunday, February 22, 2015

Mbiringanya ni mkombozi kiuchumi na kiafya:FAO Kusikiliza / Hamishia


Tunda la mbiringanya. (Picha:FAO)
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limetangaza Mbiringanya kuwa  zao la asili kwa mwezi huu wa Januari.FAO inasema majani machanga ya mbiringanya huchanganywa kwenye supu au na mboga nyingine na pia kuliwa mabichi. Halikadhalika tunda lake linaweza kutengenezwa achali au kuliwa bichi na hata kuchanganywa na nyama.
Licha ya kwamba kuna aina mbili za mbiringanya moja yenye tunda refu na nyingine tunda la mviringo, FAO inasema aina zote ni mkombozi kwa wakulima wadogo mijini na vijijini kwani hutoa mazao mengi kwenye bustani ndogo.
Tovuti ya FAO pamoja na kuelezea mapishi ya biringanya, inataja matumizi yake kiafya ikisema mizizi na matunda yake hutumika kupunguza maumivu, shinikizo la damu ilhali juisi itokanayo na majani huweza kutibu matatizo ya njia ya mkojo.

No comments:

Post a Comment