Thursday, February 26, 2015

UFUGAJI KWA UJUMLA


Ufugaji : ni neno linalotumika kumaanisha wanyama wanaofugwa na binadamu kwa malengo ya kumpatia chakula au faida Fulani. Mifugo inaweza kufugwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji madogo madogo au ufugaji wa faida wenye kuinua uchumi wa mfugaji. Wanyama wanaoweza kufugwa na binadamu ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na aina zake, njiwa, punda, farasi, kware, kanga, ngamia, na mbogo maji. Mbwa nap aka hufugwa na binadamu kwa ajili ya kumsaidia ulinzi lakini pia siku hizi hufugwa kama rafiki wa binadamu


MADHUMUNI YA UFUGAJIYapo madhumuni makubwa mawili yanayoweza kumvuta mtu fulani apende kufuga;
a) Thamani ya kiuchumi itokanayo na ufugajii.     Nyama- Nyama ni muhimu kwa ajili ya kupata protini na nguvu, mfugaji akiuza nyama au mfugo wenyewe ukiwa mzima anajipatia kipato.ii.    Maziwa na mazao yake- Kut okana na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia na mbogo maji, mfugaji anaweza kujipatia maziwa na mazao yake kama mtindi, jibini, na siagi/samuli. Maziwa na mazao haya anaweza kuyatumia katka familia lakini pia akauza kujiongezea kipato chake.iii.   Nyuzi- baadhi ya mifugo manyoa yake yanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali kama kutengenezea nguo mfano manyoa ya kuku, mbuzi, kondoo, ng’ombe. Hivyo yakiuzwa yanasaidia kuongeza kipato.iv.  Mifupa, pembe na Ngozi- Ngozi ya mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo hutumika kutengeneza viatu, nguo. Mifupa hutumika kutengenezea viatu, gundi, kuwambia ngoma, na chakula cha mifugo, wakati pembe hutumika kwa mabaragumu yanayopigwa kwenye ngoma za jadi, kutoa taarifa fulani katika jamii.v.    Mbolea ya mifugo- Hutumika mashambani kuongeza uzalishaji, kukandikia nyumba, kuchomea matofali na vyungu, pia hutumika kama kuni, na kuzalishia gesi. Mbolea inaweza ikauzwa na kumpatia mfugaji pesa kwa matumizi yake mbalmbali.vi.  Nguvu kazi-Mifugo mingi hutumiwa  na binadamu kumsaidia kufanya kazi ulani, mfano ngombe na punda  hutumika kwa ajili ya kulima, kukota mikokoteni, kuvuta miti na mizigo mingine. Punda, farasi na ngamia hutumika kama usafiri wa kusafisha watu au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine au wakati mfugaji anahama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.


b) Thamani isiyo ya kiuchumii.     Ufahari- Kuwa na mifugo kunamletea mfugaji ufahari na hivyo kumfanya awe na amani kwani hana hofu hata akiwa na matatizo anayosehemu ya kukimbilia kwa haraka bila ya kupata msongo wa mawazo.ii.    Kuwa sehemu ya familia- Wapo watu wanaofuga wanyama kwa lengo la kuwa marafiki wa karibu au kuwa sehemu ya familia, wanyama wanaofugwa kwa jinsi hii hawauzwi wala hawaliwi. Tena mnyama akiugua au kufa huduma yake inafanana sana ya mwanadamu mwenye mfugo hupata huzuni.iii.   Imani ya kidini- Wapo wanaofuga wanya kwa lengo la kuabudu kama miungu wao, mfano dini ya kihindi huabudu ng’ombe. Lakini pia mifugo hutumika kwenye imani za kimila wanapofanya matambiko au kutoa kafara kwa waganga wa kienyeji au wanapofanya mazindiko ya mali, mashamba, nyumba, au magari. Wanya wamekuwa wakitumika kwa kazi hii tangu karne nyingi zilizopiata.iv.  Kusafisha mashamba- Mifugo pia hutumika kwa lengo la kusafisha mashamba kwa kulishia mifugo kwenye mashamba ili yawe safi. Wakati mifugo inakula nyasi na majani ya shamba pamoja na kukanyaga huasidia kuua magugu na kuzuia yasiote. Njia hii si nzuri kwa upande mwingine kwa vile huharibu pia virutubisho vya shamba na kufanya litoe mazao duni.


AINA ZA UFUGAJIZipo aina kuu mbili za ufugaji, ufugaji wa kuhamahama na ufugaji wa kutulia eneo moja. Wafugaji wa jamii ya kuhamahama huhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa lengo la kuatafuta chakula, maji na kukimbia magonjwa ya mifugo. Uhamaji huu hutegemea kipindi cha mwaka, wakati wa mvua wafugaji husogea karibu na sehemu ambapo kuna makazi ya kudumu ya watu wengine kwa ajili ya urahisi wa mahitaji mengine ya kijamii. Wakati wa mvua huwa hakuna shida ya maji na chakula maeneo mengi. Wakati wa kiangazi maeneo haya majani huwa yameisha nap engine maji hakuna, hivyo huhama kwenda sehemu ambapo watapata mahitaji hayo. Ufugaji wa aina hii hufanywa kwa ng’ombe wa kienyeji tu kwani ndio wanaoweza kuvumilia joto, magonjwa na shuruti nyingine nyingi zinazopatikana wakati wa uhamaji. Wafugaji wanaofanya ufugaji huu ni wa jamii ya kimasai, kisukuma, na kibarbeiji, hawa wameshazoea kuishi porini na hawanatabia ya kujenga makazi ya kudumu kwa sababu ya kuhamahama. Hasara kubwa ya ufugaji huu ni kukosa huduma za msingi kama shule, hospitali, makanisa na misikiti. Lakini kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la watu linalofanya maeneo ya kulishia kupungua kunafanya wafugaji hawa sasa wanze kuhama kutoka aina hii ya ufugaji kuingia ile ya kutokuhamahama.Ufugaji usio wa kuhamaha unafanywa na watu wanaoishi sehemu moja kama kijiji na kufanya ufugaji wao ndani ya jamii. Hawa hufuga mifugo yao kwa kuifungia ndani muda wote na kuwaletea majani au kwa kuwachunga mchana na jioni kuwafungia ndani. Wale wanaowafungia ndani wanahitaji wakati mwingine kulima majani yatakayotumika kuwalisha mifugo yao. Hapa ufuagaji wa kisasa na wa kienyeji hufanyika kwa njia zote mbili, kuwafungia ndani muda wote au usiku tu. Huu ndiyo ufugaji wenye tija, kwani mfugaji atakuwa na mifugo michache na ataihudumia kirahisi zaidi kwa kuwapa huduma zinazotakiwa. 

No comments:

Post a Comment