Benki ya wanawake nchini TWB kwa kushirikiana na kampuni ya ufugaji wa kuku ya TWIGA FEEDS, imeanza kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wafugaji wa kuku ili kuwajengea uwezo wa kuwa na ufugaji wenye tija.
Wakizungumza kwenye mafunzo hayo , MKUU WA KITENGO CHA MIKOPO wa TWB, WALES MDOE na mkurugenzi wa TWIGA FEEDS, GREN MOSHI wamesema mafunzo hayo yanakwenda sambamba na utoaji wa mikopo ya ufugaji wa kuku kwa wajasiriamali.
Akifungua mafunzo hayo jijini DSM, mwakilishi wa WIZARA YA HABARI VIJANA NA MICHEZO DR. STEVEN KISSUI ameishauri benki ya wanawake kuongeza kiasi cha mikopo inayotolewa kwa wajasiriamali ili mikopo hiyo iweze kuwafikia wajasiriamali wengi.
No comments:
Post a Comment