Tuesday, February 24, 2015

Serikali kutoa elimu kwa wakulima wadogo wa Pamba.

Na Gloria Matola,
Pwani Bagamoyo.
Serikali imejipanga kuendelea kuwaelimisha wakulima wadogo wadogo wa zao la pamba waliopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ili wafikie hatua ya kulifanya zao hilo kuwa la kibiashara zaidi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na hali ya umasikini uliokithiri kwenye ukanda wa Mashariki.
Hayo yameelezwa kwenye ziara ya Bodi ya Pamba kwa kushirikiana na Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Pwani CORECU na TACOGA lengo likiwa ni kuwahamasisha wakulima wa zao hilo kurejea kwenye kilimo hicho.
Walipozungumza na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wakulima hao wamesema kumekuwepo na tatizo la muda mrefu la soko la uhakika hivyo kuitaka Serikali kueleza mipango yake katika kukabiliana na tatizo hilo.
Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania James Shimbe amesema Serikali imejipanga vizuri kutatua matatizo yote yaliyopo ikiwa ni pamoja na kufungua kiwanda cha kuchambua pamba cha Bagamoyo.
Naye Meneja wa chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Pwani Seif Upalla amewahakikishia wakulima hao kupata soko la uhakika ikiwa ni pamoja na chama hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi amewataka wakulima hao kuitikia mwito wa kuanza kulima zao la pamba kwa kuwa tayari wamehakikishiwa mazingira bora ya masoko.

No comments:

Post a Comment